MWALIMU MBARONI KWA UNYANYASAJI, WATETEZI WAHAKI ZA BINADAMU WATOA TAMKO;



Na makaliblog,Mara
Kituo cha msaada wa Kisheria na kijamii (LSAC) kwa kushirikiana na watetezi wengine wa haki za binadamu, waliopo Mkoani Mara, kwa sauti moja wametoa tamko la kupiga vikali, kitendo cha ukatili kilichofanywa na mwalimu Issaya wa Shule ya Sekondari Nyabisare.

Kwamba, mnamo mwezi June, 2016 mwalimu Issaya alimfata mtoto Maria Michael kutoka katika Mkoa wa Dodoma kwa makubaliano kuwa anampeleka Shule. Baada ya Mtoto huyo kusikia kuwa anapelekwa Shule, aliitikia wito huo na hatimaye akafikishwa Manispaa ya Musoma katika Mkoa wa Mara. Alipofika Mkoani Mara habari ikabadilika, mtoto Maria akawa msichana wa kazi za ndani kwa mwalimu huyo. Mtoto alipomkumbusha kuwa anahitaji shule kama walivyokubaliana mtoto aliambulia adhabu na vipigo visivyo koma, na akawa hana namna ya kufanya.

Mwezi huo huo mtoto alianzishiwa biashara ya kuuza na kutembeza nyanya mtaani kuanzia asubuhi hadi jioni na ilipotokea hajarudisha chenji au amesababisha hasara katika biashara hiyo mtoto Maria alipokea vipigo na kunyimwa chakula. Kitendo hicho kimefanyika kwa muda wa mwaka mzima kuanzia june, 2016 alipotolewa Dodoma hadi july 2017.

Ilipofika mwezi mwezi july, 2017 mtoto Maria alishindwa kuvumilia, alitoroka na akakutwa mtaani na wasamaria wema ambao walitoa taarifa katika kituo cha Watoto Wapinge UKIMWI, kituo cha msaada wa sheria na jamii (LSAC) na kituo cha jipe moyo na kwa kushirikiana na wadau wengine watetezi wa haki za binadamu tulianza kufuatilia kwa ukaribu suala hili.

Ambapo tukatoa taarifa polisi, mtoto akapatiwa hifadhi (jipe moyo) na harakati za kumtafuta mtuhumiwa ziliendelea, tarehe9.8.2017 kwa kushirikiana na polisi mtuhumiwa na kuwekwa chini ya ulinzi.

Kwa ujumla kitendo alichofanyiwa mtoto, kitendo cha kusafirishwa toka Dodoma kuja Musoma, (human trafficking), kufanyishwa kazi na kupigwa kutukanwa na mwalimu pamoja na mke wake mwalimu (Issaya) bila hata huruma, ni kitendo cha uonevu, hakikubaliki katika jamii, ni kitendo ambacho ni kinyume na sheria na haki za binadamu. Kinachotakiwa kukemewa kwa nguvu zote. Tanzania inaongozwa na sheria;



Lakini pia tukumbuke kuwa; Tanzania ni wanachama wa umoja wa mataifa na kuna mikataba ambayo Tanzania imesaini na baadaye sheria zimetungwa ili kutekeleza matamko hayo, hii ikiwa ni pamoja na matamko ya kulinda na kutetea haki za binadamu Tamko la umoja wa kimataifa kuhusu haki za binadamu la mwaka 1948.

Powered by Blogger.