RASMI; HIZI HAPA JEZI WATAKAZOTUMIA YANGA NA SIMBA LIGI KUU VPL;


MSEMAJI wa Simba, Haji Manara aliwaacha hoi wadau waliohudhuria hafla ya ugawaji wa vifaa kwa timu zinazoshiriki ligi kuu ya Vodacom baada ya kusimama kama mwakilishi wa Yanga.

Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom leo imegawa vifaa vyenye thamani ya sh 500 milioni kwa timu 16 zinazoshiriki ligi kuu ikiwa ni wiki tatu kabla ligi haijaanza.

Katika hafla hiyo vijana waliovalia jezi za kila timu walikuwa wakipanda jukwaani kuonyesha jezi hizo huku katikati yao akisimama mwakilishi wa klabu husika.



Kwa bahati mbaya hakukuwa na kiongozi yeyote wa Yanga katika hafla hiyo ndipo Manara alipoinuka na kwenda kusimama kama mwakilishi wa mabingwa hao watetezi.

Jambo hilo liliwafurahisha watu wengi waliohudhuria hafla hiyo hali iliyopelekea walipuke kwa vicheko ukumbini hapo.

Simba na Yanga zitakutana Agosti 23 kwenye mechi ya ngao ya hisani kuashiria kufunguliwa rasmi kwa pazia la ligi hiyo.


PICHA NA BOIPLUS
Powered by Blogger.