BENKI YA FINCA MICROFINANCE YAZINDUA KAMPENI YA FIKANAFINCA
Meneja wa Masoko wa Benki ya Finca Microfinance Bw. Nicholous John,
Benki ya FINCA Microfinance Bwana Nicholous John akionyesha mfano wa
tiketi ya ndege itakayotumika katika kampeni yao iliyopewa jina la
FikaNaFINCA iliyozinduliwa jana jijini Dar es Salaam. Pembeni yake ni
Afisa Mawasiliano wa Shirika la ndege la Tanzania ATCL Bi. Lilian
Fungamtama .
Kutoka kushoto ni Meneja usafirishaji wa kampuni ya Super Feo Bw
Masumbuko akifuatiwa na Meneja wa Masoko wa Benki ya Finca Microfinance
Bw. Nicholous John, Afisa Mawasiliano wa Shirika la ndege la Tanzania
ATCL Bi. Lilian Fungamtama Bi. Lilian Fungamtama na Mtaalamu wa Masoko
wa Benki ya FINCA Bw. Noel Mulumba wakionyesha mifano ya tiketi za
usafirishaji ambazo wateja watapaswa kupiga picha na kushirikisha
wafuasi wako katika mitandao ya kijamii ili kujishindia tiketi ya bure
katika kampeni iliyopewa jina la FikanaFINCA
****
Dar es Salaam, Agosti 2, 2017-Moja ya Benki inayokua kwa kasi nchini,
Benki ya FINCA Microfinance, leo imetangaza kampeni ya miezi miwili
inayofahamika kama 'FikaNaFINCA' Kampeni hii itampa fursa
anayefwatilia kurasa za kijamii ya benki hiyo nafasi ya kujishindia
tiketi ya kwenda na kurudi bure baada ya kuposti picha ya bahasha ya
tiketi yenye nembo ya FIKA NA FINCA na pia kupendwa na watu wengi.
Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari katika makao makuu ya
benki jijini Dar es Salaam, Meneja wa Masoko wa Benki ya Finca
Microfinance, Nicholus John alisema kuwa washindi watakuwa na nafasi ya
kupata tiketi za usafiri wa anga na barabara ya kwenda na kurudi kutoka
mashirika ya usafiri wa anga ya ndani ya Air Tanzania (ATCL) na Auric
Air na pia kwa mabasi yanayoenda bara yakiwemo mabasi ya kampuni za
Ngorika, New Force na Isamilo.
"FINCA inathamini wateja wake na jamii kwa ujumla, katika kuonyesha
hilo, ndiyo maana tumeleta kampeni hii itakayoenda kwa miezi miwili huku
mshindi kutangazwa kila wiki. Jinsi ya kushinda ni rahisi sana, piga
picha tiketi yako yenye nembo ya FIKA NA FINCA, posti kwenye kurasa ya
Facebook na Instagram ukiweka #FikaNaFINCA kwenye caption, alafu aalike
ndugu jamaa na marafiki kuipenda."alisema John.
John aliongeza: "Ninatoa wito kwa Watanzania kuchukua fursa hii ya
kipekee na kushiriki kwa wingi ili kushinda ofa hii ya kusafiri bure".
Kwa upande wao, Air Tanzania, Lilian Fungamtama ambaye ni Afisa
Mawasiliano wa ATCL aliipongeza benki hiyo kwa kuwaunganisha pamoja ili
kuwapatia abiria wao safari za bure ambayo wanaamini itaimarisha
uhususiano mzuri na wateja wao.
Benki ya FINCA Microfinance, inafurahia kuwa na matawi zaidi ya ishirini
pamoja na mawakala zaidi ya mia nchi nzima. Benki hiyo pia inajivunia
huduma zake za kuweka akiba na kutoa mikopo yenye riba nafuu.
Benki hiyo inaamini huduma zake zinasaidia wateja wao kufikia malengo
chini ya msaada na usimamizi wao na ndo sababu ya msingi ya kuja na
kampeni hii ya FikaNaFINCA.

