MWALIMU APANDISHWA KIZIMBANI KWAKUPOKEA RUSHWA YA TSH.30,000 MARA.



Na makaliblog, MARA.
Taasisi ya kuzuia nakupambana na Rushwa Mkoani Mara imemfikisha katika Mahakama ya Wilaya ya Bunda Mwalimu Samwel Johnson Owawa (29yrs) kwa makosa ya kudai kupokea rushwa ya shiingi elfu thelathini.

Samwel Johnson Owawa ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nyambitilwa iliyoko katika kijiji cha Misisi kata ya Sazira Wilaya ya Bunda na Mkoa wa Mara.

Aliomba na kupokea rushwaya shilingi elfu thelathini toka kwa mzazi (Jina linahifadhiwa) wa mtoto anayesoma darasa la pili katika Shule hiyo (Jina linahifadhiwa) ili asichukue hatua za kisheria dhidiya mzazi huyo kwa kosa la utoro wa mwanae.

Awali wakati wa likizo ya mwezi juni 2017 mtoto huyo wa darasa la pili na baba yake walienda Mkoani Kagera kusalimia ndugu na jamaa, hata hivyo hawakuweza kurejea mapema hadi shule zikafunguliwa kutokana na kuugua kwa mtoto huyo wakiwa MkoaniKager.

Baada ya mtoto huyo kupata nafuu walirejea Bunda na mtoto akaenda shule kwa nia ya kuendelea na masomo yake, hata hivyo alipofika shule alirejeshwa nyumbani na kutakiwa kuja na mzazi wake.

Baba wa mtoto aliitika wito na alipoonana na mwalimu Owawa alitakiwa atoe rushwa yaelfu thelathini ili mtoto huyo aweze kuendelea na masomo la sivyo atachukuliwa hatua za kisheria dhidi ya mzazi huyo.

Mzazi aliahidi kutafuta fedha hizo, hata hivyo ilipofika 31, julai 2017 mtoto alifukuzwa shule ikiwa ni shinikizo la Mwalimu Owawa kwa mzazi kutekeleza ahadi ya rushwa ya elfu thelathini kama walivyokuwa wamekubaliana.

Mzazi huyo hakuwa na fedha hizo, hivyo akaona atoe taarifa TAKUKURU ambapo mtego wa hongo hiyo uliandaliwa, Mwalimu Owawa alikamatwa na maafisa wa TAKUKURU akiwa amepokea elfu thelathni za mtego wa rushwa na hivyo kufikishwa Mahakamani Agost 1, 2017.

Kesi hiyo ya rushwa namba CC 292/2017 ipo mbele ya hakimu Mfawdhi wa Mahakama ya Wilaya ya Bunda Mheshimiwa Jackline Rugemalira, imefikishwa Mahakamani hapo na mwendesha mashitaka wa TAKUKURU Martin Makani.
Mshiakiwa alikana makosa yake, yuko nje kwa dhamama na baada ya kutimiza masharti yaliyowekwa na mahakama hiyo, uchunguzi wa jalada hilo uko tayari na kesi hiyo imepngwa kwa ajili ya usikilzwaji wa awali 9, Agoditi 2017.

Ni wito wetu wananchi wasiwe na woga wa kutoa taarifa za rushwa TAKUKURU, ni wajibu wetu kufanyia kazi kila taaifa inayotufikia na kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wahusika pasipo kujali hadhi, kabila, dini au wadhifa wa watu.
                 
                TUPE MAONI YAKO KWA HABARI NA MTUKIO TUPIGIE KUPITIA 0754295996
                    UNAWEZA KUTANGAZA NASI KUPITIA mussaj970@gmail.com
Powered by Blogger.