MKURUGENZI WA MAMLAKA YA MAJI MUSOMA (muwasa) MBARONI KWA RUSHWA



Na MAKALIBLOG.MARA
Tasisi ya kuzuia na kupambana na rushhwa mkoani Mara imemfikisha katika mahakama ya wilaya musoma mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira musoma MUWASA) Hawaiju said Gantala.

Katika kosa la kwanza hadi la tano hawaiju saidi gantala anashitakiwa kwa kughushi nyaraka za kuingiziwa mshahara (salary slip) za mwzi a septemba na Desemba 2014 na akaghushi nyara za kuingizia mshahara (salary slip) za mwezi june,julai na Agost2016 kuonyesha kwamba ninyaraka halali kutoka MUWASA huku akifahamu sio kweli.

Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Mara Holle Makungu amesema Kesi hiyo ya jina namba cc179\2017 iko mbele ya Mh Hakimu karimu mushi na imefikishwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Moses Malewo.

Gantala Hawaiju anashitakiwa kwa makosa ya kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kuwasilisha nyaraka za kupotosha katika Benki za CRDB na NBC matawi ya Musoma.

Katika kosa la sita Hawaiju Gantala anashitakiwa kwa kujipatia shilingi Milioni thelathini na (Tshs. 30,000,000) kutoka bank ya CRDB tawi la musoma kama mkopo kwa kutumia nyaraka za kuingizia mshahara (salary slip)za uongo zilizoonysha kwamba katika mwezi septemba na Disemba mwaka 2014 mshahara wake wake ulikuwa shilingi million mbili laki saba sitini na saba elfu miatano arobaini na tisa (Tshs.2,767,549/=) huku akijua kuwa haikuwa kweli kujipatia fedha ambazo hakustahili.

Katika kosa la saba Hawaiju said Gantala anashtakiwa kujipatia shilingi thelathini natatu milioni na laki nne (Tshs. 33,400,000) kutoka benki ya NBC tawi la Musoma kama mkpo kwa kutumia nyaraka za kusingiziwa za mshahara wa mtumishi za uongo (salary slip) zilizoonyesha kuwa kaika mwezi juni julai na Agosti 2016 mshahara wake ulikuwa shilingi milioni mbili na laki sita mia moja sabini na tisa na senti themanini na mbili (Tshs.2,636,179.82/=) huku akijua kuwa haikuwa kweli hivyo kujipatia fedha hizo bila kustahili.

Katika kosa la nane hadi la 13 Mtuhumiwa anashtakiwa kwa kuwasilisha nyaraka za kusingiziwa mshahara wa watumishi wa uongo (salary slip) katika Benki za CRDB na NBC matawi ya Musoma akidanganya kuwa zilikuwa nyaraka halali kutoka MUWASA, kwa kutumia nyaraka hizo za kupotosha aliweza kujipatia jumla ya shilingi sitini na tatu milioni na laki nne (Tshs. 63,400,000/=) toka benki hizo za CRDB na NBC matawi ya Musoma.

Katika shtaka la 14 mshtakiwa anashtakiwa kwa kosa la kumlaghai Mkuu wa Idara ya Utwala MUWASA Brian D Moshi kuweka saini hati za kuingiziwa mshahara wa mtumishi za kughushi (salary slip) kwa mwezi Juni, Julai na Agosti mwaka 2016 ili zionekane kuwa ni hati halali kutoka Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira ya Musoma huku akijua siyo nyaraka halali zililenga kupotosha Taasisi za fedha.

Katika shtaka la 15 mshtakiwa ana shtakiwa Issaya Maswi Nyaiho ambaye ni Mkuu wa Idara ya Fedha MUWASA kutia saini hati za kusingiziwa mshahara wa mtumishi (salary slip) za kughushi za miezi Septemba, Oktoba na Novemba mwaka 2014 ili zionekane kuwa ni hati halali na zililenga kupotosha Taasisi za Fedha.

Mshtakiwa alikana kutenda makosa hayo na yuko nje ya dhamana kwa wadhamini wawili kila mmoja kuweka hati ya mali isiyohamishika yenye thamani kama hiyo, kesi hiyo itatajwa tena mahakamani hapo Agosti 22, mwaka 2017.

Powered by Blogger.