BABA AOMBA MSAADA BAADA YA MKEWE KUJIFUNGUA WATATO WATATU MARA,DAKTARI ASIMULIA;



Na Makalaiblog,Mara
Baba wa watoto watatu Mkazi wa Manispaa ya Musoma mkoani Mara ameiomba jamii pamoja na serikali kutoa msaada wa kuwalea watoto watatu ambao mkewe amejifungua kutokana na maisha yake ya duni.

Baba huyo wawatoto watatu aliyetambulika kwa jina la Elisha Masatu aliwashukuru madaktari wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa mara kwa huduma waliompa mkewe kutokana na kufika hosptalini hapo Siku ya Jumamosi akiwa hajitambui.

“Natoa shukrani kwa wahudumu wa hosptali hii ya rufaa ya mkoa wa mara kwani wamejitahidi kuokoa uhai wa mke wangu kutokana na kuletwa akiwa katika hali ambayo ni tata na vipimo kuonesha ana mimba ya watoto watatu,” alisema.

Happy silasi ambaye nimzazi wawatoto hao amefikisha watoto saba kwa nzao nne, nzao yakwanza alijifungua mtoto mmoja na nzao ya pili mapacha wawili na nzao yatatu akajifungua motto mmoja ambapo sasa inafikishajumla ya watoto saba.

Bi.silasi kwa sasa maziwa hayatoshi kifuani kutokana na lishe duni kwake imemladhimu kutumia maziwa yang’ombe maalumkwa makuzi ya nalisehe ya watoto hao.

Bi.Neema mganga ambae ni kiongozi wawodi ya wazazi katika hospitali ya rufaa mjini musoma alifafanua kuhusu tatizo alilonalo mzazi huyo kuwa ni ugumu wamaisha jambo lililosababisha kumkatisha tama baada ya vipimo kuonesha anawatoto watatu.

“tumempokea siku ya jumamosi akiwa na maumivu makalindipo tukampeleka katika vipimo tukabaini anawatoto watatu lakinimtoto mmoja kati yahao watatu alikuwa amekaa vibaya lakini hakuwa tiari kupokea kwa furaha taaria hizo baada ya ushauri tukamfanyia upasuaji nakuwatoa wawatotohao wakiwa wenye afya njema,’’ alisema kiongozi huyo.

Aidha,alitoa rai kwa yeyeyote mwenye uwezo wakumsaidia mzazi huyo kwa ajiri ya malezi ya watoto hao kwa mavazi,fedha,na chakula kwaajiri ya watoto nae yeye wajitokeze kumsaidia mama huyo.

USHAULI MAONI TUPIA HAPA MATUSI (HAPANA) TUCHEKI NA 0754295996
mussaj970@gmail.com mussayohanna@yahoo.com

Powered by Blogger.