MAKALIBLOG.VIDEO MTIZAME RAIS WA ROTARY CLUB MUSOMA AKIZUNGUMZA;DEAR FOUNDATION KUPITIA MRADI WA ACLIWOPA WAENDELEA KUWANUFAISHA WATU WE...
picha ni Rais wa ROTARY CLUB MUSOMA Deogratius Wegina akipresent Mradi wa ACLIWOPA unaodahimiwa na DEAR Foundation mara,.
Na MAKALIBLOG.MUSOMA
Zaidi ya vikundi 30 vimefaidika na mradi unaofadhiliwa na DEAR foundation kutoka swirtzerland kupitia mradi wa ACLIWOPA katika wilaya ya Musoma mkoani mara ambapo mpaka sasa kiasi cha shilingi milioni 45 zimetolewa ilikuwasaidia wanawake na watu wenye mahitaji maalm ya (Alibino).
Akizungumza na makaliblog Rais wa Rotary club Musoma Bw.Deogratius wegina amesema pesa hizo mpaka sasa toka zimetolewa zimeonyesha maendeleo mazuri kutokanana walengwa kuzitumia inavyotakiwa.
Kupitia DEAR Foundation mpaka sasa akina mama 150 Wamenufaika na mradi huo ambapo mpaka sasa wanaufugaji wa kuku,uanzishaji maduka,kushonana uselemala na kufanya biashara ndogo ndogo za ujasilia mali ambapo kila kikundi kimoja kati ya vikundi thelathini wanawapatia kiasi cha shilingi milioni mmoja la Nnusu kila kikundi kwa masharti nafuu ikiwa wanapewa kwa imani yao wenyewe ya kurudisha.
Wegina amesema wamekuwa wakitoa elimu kabla ya kuwapatia pesa hizo ilikuondoa na kuwaelekeza matumizi mazuri ya pesa hizo ambapo wanatumia semina kupitia misaada ya ROTARY ilikutafuta wakufunzi ambao watawasaidia kuwafundisha kuhusiana na matumizi ya pesa hizo kwani inatolewa kwa kikundi na sikwa mtu mmojammoja.
Amewataka kuzitumia vyema pesa hizo kuliko kuanza kuzitumia kwa ajiri ya starehe bali watumie kwa malengo yaliyowekwa kwa ajili ya pesa hizo.
Kutoa msaada huo nijuhudi ya kuunga mkono serikali ya tano ambayo moto wake nimhimili wa viwanda hivyo itasaidia kuanzisha viwanda vidogovidogo.