MWENYEKITI WA CCM AWAONYA VIONGOZI WANAOPANGA SAFU ZAO ZA WAGOMBEA;



Mwenyekiti wa CCM Wilayani Rorya Mkoani Mara Samwel Kiboye N03 akisisitiza  katika kikao hicho kilichofanyika kata ya Bukwe kwa lengo la kutoa maelekezo ya chama pia Mwenyekiti huyo amewaomba wanachama kuondoa tofauti zao na  makundi katika harakati hizi za uchaguzi Ngazi ya Kata Wilaya Mkoa hadi Taifa kwa lengo la kulinda heshima ya chama huku akipongeza juhudi za Rais katika kazi yake.

Katibu wa Chama cha Mapinduzi( CCM) Mkoa wa Mara Innocent Nanzabar akiongea na viongozi wa chama hicho katika kata ya Bukwe Wilayani Rorya Mkoani Mara ni katika ziara yake aliyoanza hii leo kwa lengo la kutoa maagizo kwa viongozi ngazi ya Shina na Tawi waliochaguliwa.


Katibu wa CCM Mkoa wa Mara Innocent uadirifu katika ngazi zao za mashina



Katibu wa CCM Wilayani Rorya Rucy Bonephace akiteta jambo na katibu wa CCM Mkoa wa Mara
Mwenyekiti wa CCM Wilayani Rorya Mkoani Mara Samwel Kiboye N03 akisisitiza jambo katika kikao hicho kilichofanyika kata ya Bukwe kwa lengo la kutoa maelekezo ya chama pia Mwenyekiti huyo amewaomba wanachama kuondoa tofauti zao na makundi katika harakati hizi za uchaguzi Ngazi ya Kata Wilaya Mkoa hadi Taifa kwa lengo la kulinda heshima ya chama huku akipongeza juhudi za Rais katika kazi yake.
Katibu UWT Mkoa wa Mara Irimina Mushongi akisisitiza akina mama kujitokeza katika chaguziKatibu wa wazazi CCM Mkoa wa Mara Robert Manjebe akisisitia suala zima la wazee kuendelea kushauri vyema chama huku vijana wakipata nafasi mbalimbali za uongozi katika chama hicho

Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilayani Rorya Mkoani Mara Samwel Kiboye NO3 akiteta jambo na Katibu wa CCM Mkoa wa Mara Innocent Nanzabar kulia ni Katibu wa CCM Wilayani Rorya Rucy Boniphace





WANANCHAMA WA SHINA


viongozi wa Ngazi ya Mashina ,Mabalozi na Matawi kata ya Bukwe Wilaya ya Rorya Mkoani Mara , wamekishukuru Chama cha Mapinduzi Taifa kwa kuona umuhimu wao kwani ndo alama na nguzo ya chama hicho kukijenga kwaajili ya ushindi wa uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 .

hayo wameyasema walipotembelewa na Katibu wa CCM Mkoa wa Mara ambaye yuko katika ziara ambayo ameambatana na Sekretarieti yake ya mkoa , kuwaeleza mabadiliko ya katiba sambamba na kuwapongeza kwa kuchaguliwa katika nafasi hizo za chama.

wamesema kuwepo kwa nafasi hizo za mabalozi na mashina chama kinaashiria uhai wa chama hicho ambapo pia wameahidi kuvuna wanachama wengi kupitia hamasa na wengi wamejitokeza kwa kutambua mabadiliko ya katiba ambayo yataleta tija kubwa kwa ustawi wa chama hicho.

mwenyekiti wa ccm wilaya ya Rorya Samweli Kiboye amewaonya viongozi kupanga safu na badala yake kila mtu mwadilifu apewe fursa ya kugombea ,kisha akaipongeza bajeti 2017/18 ambayo imekithi mahitaji ya wananchi hasa katika ushuru wa mazao na magari .

Kwa upande wake katibu wa ccm mkoa wa Mara Innocent Nanzabar amesema kuwa sekretarieti ya CCM Mkoa imejipanga kukutana na viongozi hao ngazi Mashina ,Mabalozi na Matawi kutoa maelekezo ya chama taifa juu ya mabadiliko ya katiba kwani wao ni alama ya chama hicho.

Katibu wa uvccm mkoani wa mara Hassan moshi akazikumbusha halmashauri kuhusu asilimia 5 za vijana na asilimia 5 ya wanawake ambayo ni haki yao ya msingi

Baada ya kumalizika uchaguzi wa ngazi hizo za mashina ,balozi na matawi tayari juni 13 wameanza kuchukua fomu kwaajili ya uchaguzi ngazi ya kata za chama hicho wilayani rorya.

Powered by Blogger.