Makamu wa Rais akemea Mimba za utotoni, awavaa Maofisa Ardhi asema serikali itatatua changamoto ya Maji Tanzania pia awataka viongozi kusimamia ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Serengeti


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameuagiza uongozi wa wilaya ya Serengeti na wa mkoa Mara kukamilisha haraka awamu ya kwanza ya ujenzi wa hospitali ya wilaya hiyo ili kuondoa adha ya wananchi kusafiri kwenda mikoa ya jirani ya Arusha na Mwanza kwenda kupata huduma afya.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa agizo leo 6-June-2017 kwenye mkutano wa hadhara mjini Mugumu wilayani Serengeti mkoani Mara mara baada ya kutembelea ujenzi wa hospitali hiyo ya wilaya na kuweka jiwe la msingi.

Makamu wa Rais amesema kutokana na wilaya ya Serengeti kupata wegeni wengi kutoka nje ya nchi ambao wanaenda kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti hivyo ni muhimu kwa viongozi wa wilaya na mkoa kwa ushirikiano na wadau wa maendeleo kukamilisha ujenzi huo haraka ili wananchi waweze kupata huduma za afya za uhakika katika wilaya yao.

Makamu wa Rais amesema kukamilika kwa ujenzi huo wa awamu ya kwanza kutaondoa taabu kubwa wanayopata wananchi wa wilaya ya Serengeti katika kupata huduma ya afya karibu na maeneo yao.

Katika kuunga mkono jitihada hizo za ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Serengeti, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ameahidi kuchangia kiasi cha shilingi milioni Tano na amewaahidi wananchi wa wilaya ya Serengeti kuwa atakikisha fedha kutoka Serikalini ambazo zinatakiwa kupelekwa wilayani humo zinapelekwa haraka ili kukamilisha ujenzi huo.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan pia amewataka wananchi kote nchini kuunga mkono jitihada za Serikali za kupambana na rushwa na ufisadi ili kuhakikisha miradi inayotekelezwa inakuwa na manufaa kwa wananchi wote.

Amewaomba wananchi nchini wasirudi nyuma katika mapambano dhidi ya rushwa bali waendelee kubaini watu wanaofanya vitendo hivyo ili Serikali iweze kuwachukulia hatua kali za kisheria .

Kuhusu tatizo la mimba mkoani Mara, Makamu wa Rais ameonyesha kuchukizwa na vitendo hivyo na kuomba vyombo vya dola na wananchi kwa ujumla kushirikiana katika kukomesha mimba za utotoni mkoani Mara.

Kwa upande wake, Mkuu wa mkoa wa Mara Dkt Charles Mlingwa amemhakikishia Makamu wa Rais kuwa maelekezo yote anayoyatoa katika ziara yake yatafanyiwa kazi ipasavyo ili kuondoa kero na changamoto zinazowakabili wananchi.

Mkuu huyo wa mkoa wa Mara ameomba wananchi wa Mkoa wa Mara kuwepa pembeni tofauti zao za kisiasa bali washirikiane na Serikali katika utekelezaji wa miradi yao ya maendeleo.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan bado anaendelea na ziara yake ya kikazi mkoani Mara ambapo hapo kesho atafanya ziara katika wilaya za Butiama na Musoma mkoani Mara.





Mkuu wa wilaya ya Serengeti Nurudin Babu akisoma taarifa kwa Makamu wa Rais
 
Makamu wa Rais akipanda Mti katika Hospitali ya Wilaya inayojengwa 
 
Mkuu wa Mkoa wa Mara Dkt Charles Mingwa akipanda Mti
Makamu wa Rais akiweka jiwe la Msingi katika ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara. 
 
 
Wakati hu huo Wananchi walipiga kelele wakati Mkuu huyo wa wilaya  akitoa taarifa ya wilaya kuhusu chakula kwa Makamu wa Rais,wakati akiwa kwenye ziara ya kutembelea wilaya hiyo kusikiliza kero,kuangalia miradi ya kimaendeleo na kutoa shukurani za kuwapa ushindi chama tawa(ccm) kuongoza nchi katika viwanja vya Mbuzi mjini Mugumu.
Wananchi hao walisikika wakisema kuwa hali ya chakula ni mbaya,hata kama serikali imetoa chakula cha msaada,na kwamba walimtaka aombe kuongezewa chakula cha msaada ambacho kitauzwa na serikali wenyewe badala ya kuwaruhusa wafanya biashara kununua chakula hicho kwa bei nafuu na kukiuza kwa bei elekezi.
Mwananchi mmoja mjasilia mali Robi Nyamuhanga alisema ni kweli serikali ilitoa chakula cha msaada ambacho walinunua kwa bei ya Tsh. 700 kwa kilo moja kwa maeneo ya mjini na vijijini kwa Tsh.750,lakini chakula hicho watu walinunua kwa siku tatu tu.
Nyamuhanga alisema baada ya siku tatu chakula kile kilichukuliwa na wafanyabiashara ambao waliuza kwa bei elekezi kwa siku mbili,baada ya hapo walipandisha bei na kuuza kwa Tsh. 21,000 kwa debe tofauti na serikali ilikuwa Tsh.14,000.
Awali Mkuu wa wilaya Baabu alisema kuwa hali ya chakula wilayani humo ni ya kuridhisha kufuatia kuwepo kwa mvua za kutosha na kwamba baada ya mda mfupi watavuna.
Baabu alisema serikali ilitoa chakula cha msaada Tani 400 ambazo walizigawa kwa kuziuza kwa bei nafuu,ambapo wananchi walifanikiwa kukinunua na kutunza akiba.
Mbunge wa jimbo hilo Marwa Ryoba alisema wilaya ya Serengeti ni wilaya ya chakula ambayo hulisha mkoa kwa kuzalisha chakula kingi,nakwamba hali ya upungufu wa chakula kwa sasa imetokana na ukame kufuatia mvua kutonyesha kwa wakati msimu wa kilimo mwaka jana na mwaka huu mwanzoni.
Hata hivyo Ryoba alimpongeza mkuu wake wa wilaya kuwa hufanya kazi kwa ushirkiano na wananchi wote sanjari mbunge bila kujali itikadi za kisiasa hali ambayo inaifanya wilaya hiyo kuwa mstari wa mbele kimaendeleo mkoani Mara.
Makamu wa Rais Samia Suluhu aliwataka wananchi kuacha kupiga kelele kuhusu hali ya ukame kwani kunyesha mvua na kutonyesha ni mapenzi ya Mungu,hivyo hakuna kiongozi aliyezuia mvua kunyesha,aliwataka kufanya kazi kwa bidii bila kukata tama.
“Hata kama kuna njaa sio kwa kiasi hicho mlichopiga kelele,ila njiani nimeona mashamba makubwa nina uhakika mtavuna hivi karibuni na tatizo la njaa litakwisha.
Powered by Blogger.