BASI LA WIBONELA LA DAR - KAHAMA LIMEGONGANA NA BASI LA TAKBIIR KIBAIGWA

  Basi la Wibonela Express lenye namba za usajili T158 CEX lililokuwa linatoka Dar es salaam kuelekea Kahama mkoani Shinyanga limegongana na basi la Tak-biir lenye namba za usajili T818 CYQ katika eneo la Kibaigwa mkoani Dodoma ambapo ujenzi wa barabara unaendelea.


Taarifa za awali zinasema watu kadhaa wamejeruhiwa.

Baadhi ya abiria waliokuwa kwenye basi la Wibonela wanasema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wao ambaye alikuwa anaendesha basi kwa mwendo kasi na hakujali malalamiko ya abiria wake kila walipomwambia apunguze mwendo.

"Hii ni mara ya pili,ya kwanza tulinusurika kupata ajali,alikuwa anaovatek 'anajaribu kuyapita magari mengini' bila  kuchukua tahadhari,ukiwaambia wanakuwa wabishi",wamesema.

Powered by Blogger.