WADAU WAKAHAWA WATOA MAAMZI YA PAMOJA KUBORESHA KAHAWA ILI KUKUZA SOKO LAO NDANI NANJE YA NCHI;

 Image result for PICHA YA KAHAWA
 Na Mwandishi wa MAKALIBLOG; Mara.
Wadau wa kilimo cha kahawa kanda  ya  mara wameazimia Kwa pamoja kuboresha  ubora wa kahawa yao ili kukuza soko LA bidhaa hiyo Katika soko la ndani na njee .

Azimio hilo lilipitishwa Katika kikao cha pamoja kilicho husisha wakulima , wataalamu wa kilimo na maafisa biashara pamoja na viongozi Wa serikali kilicho fanyika Jana katika ukumbi Wa uwekezaji uliopo katika ofisi za mkuu wa  mkoa.
Naye afisa kilimo wa  mkoa nyakisida Denis amesema kuwa ni wakati sasa wa kutoa elimu kwa wakulima na vyama vya msingi kwa kuwasaidia ili kuweza kuboresha mfumo utakao wezesha kutoa mapato ya zao la kahawa kwa wakati muafaka.
Kwa upande wake Afisa biashara gambales  timotheo aliwaaasa  viongozi wa vyama vya ushirika kuwa wawe wabunifu katika kuboresha zao lao na kuweza kupata zao lenye ubora unao takiwa na wenye tija.
Aidha kwa upande wake mkuu wa wilaya ya geita Herman kapufi amesema kuwa atashirikiana vyema na wakulima ili waweze kupata miche bora nakuwatafutia soko la uakika wakulima wa zao la kahawa wa wilaya yake.

Powered by Blogger.