Mkuu wa wilaya ya Tarime Luoga akionesha jinsi wanavyojenga
vibaya Nyumba hizo amesema kuwa kuna haja kubwa ya kujenga nyumba imara
NA MAKALIBLOG;
Kutokana na mvua ambazo
zinaendelea kunyesha wananchi wa kijiji cha Murito Kata ya Kemambo Wilayani
Tarime Mkoani Mara wamekumbwa na maafa ya kuezuliwa Nyumba na baadhi kubomolewa
takribani Nyumba 52 zimeezuliwa zikiwemo nyumba 25 za bati.
Mkuu wa wilaya ya Tarime Glorius
Luoga ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya Maafa wa Wilaya ametembelea eneo hilo na kuwapa pole
wananchi ambao wamekumbwa na tatizo hilo.
“Nimemwagiza mtendaji wa kijiji
kuorodhesha kwa usahihi nyumba zote za wananchi zilizobomolewa, na hali ya
wananchi hao ambao hawana uwezo kabisa ili niweze kukaa viongozi wa hata kama
tutawaacha hivi hawataweza kupata jinsi ya kujisaidia kupata pa kujisitili,”
alisema Luoga.
Eneo hilo lina chumvi hivyo miti
iliyojenga nyumba hizo zinalika haraka hivyo, hivyo kuwataka wananchi kupanda
miti ya asili ambayo inastawi katika eneo hilo ili kuweza kuimarisha ulinzi wa
nyumba zao.
“Eneo hili halina miti mingi
kutokana na wakazi wake kuwa na mifugo mingi inayoharibu miti hiyo, ni vyema
tukapanda miti ili kusaidia kuzuia upepo mkali unaotokea,” alisema Luoga.
Maeneo yaliyokumbwa na dhahama hiyo
ni vitongoji vya Moroko Senta, Maabera, Kumichongoma, Kesankwe na Keghati
katika kijiji cha Murito
Diwani wa kata ya Kemambo Rashid Bugomba alisema watu
wanalala nje kutokana na madhara yaliyotokea katika eneo hilo la Mrito huku
akiomba serikali kutoa msaada wa hali na mali.
“Nyumba
nyingi zilizoezuliwa na makanisa yameezuliwana na tunaomba msaada mkubwa wa
kibinadamu ili kuwasaidia wananchi hao, kwa uwezo wetu tutajitahidi kuwasaidia
tutakavyoweza lakini pia majirani waendelee kuwasaidia wenzao,” alisema
Bogomba.
Wananchi waliokumbwa na tatizo hilo
waliomba serikali kuwapa msaada wa hali na mali ili wapate sehemu ya kujihifadhi
ambapo mwenyekiti wa kijiji cha Murito
alieleza kuwa hali ni mbaya.
“Jumla ya kaya 52 zimeharibiwa na
mvua iliyoambatana na upepo mkali, na kuwafanya wananchi wangu kulala nje kwani
hawana pa kuishi katika kipindi hiki kwa kuwa hata maghala ya chakula
yaliangushwa na upepo kutokana na kuwa mkubwa,”alisema Zephania Mahati
mwenyekiti wa kijiji cha Murito.
Mwisho.
 |
Baadhi ya Nyumba za wananchi wakazi wa kijiji cha Murito Kata ya
Kemambo wilayani Tarime Mkoani Mara zikiwa zimeezuliwa na Mvua ambayo
iliambatana na upepo mkali kaya takribani 52 zimekumbwa na tatizo hilo
Nyumba zabomolewa na kuezuliwa.
|
 |
Mkuu wa wilaya ya Tarime Glorious Luoga aliyevaa suti nyeusi akionesha moja jengo ambalo limeezuliwa na upepo mkali.
|
 |
Nyumba zilizoezuliwa na upepo kijiji cha Murito
|
 |
Mmoja wa wananchi akieleza juu ya maafa hayo.
|
 |
Mkuu wa wilaya akieleza jinsi ya kujenga nyumba bora.
|
 |
Mti ulivyodondoka na upepo mkali
|
 |
Nyumba ambayo imebomolewa
|
 |
Bibi ambaye amekumbwa na changamoto hiyo.
|
 |
Diwani wa kata ya Kemambo Rashid Bugomba akisalimia bibi ambaye amekumbwa na janga la kubomoka kwa nyumba yake.
|