MASKAUTI WATUME YA TAIFA YA UCHAGUZI NEC WATUA MKOANI MARA;

KUSHOTO NIMKUU WA MSAFARA BWANA SULEMANI BALULA KATIKATI NI 
STEPHEN ELISANT NA PEMBENI YAKE  NI JOSEPH  CHAROS NI MASKAUTI WATUME YA UCHAGUI NEC WAKIWA KATIKA STUDIO ZA VICTORIA RADIO KUFIKISHA ELIMU YA MPIGA KURA MKOANI MARA.


NA MAKALIBLOG; MUSOMA,MARA
Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC imefika mkoani mara kwa ajiri ya kuendeleza zoezi la utoaji Elimu ya mpiga kura ikiwa nizoezi endelevu kwa nchi nzima nakuifikisha Elimu ipasavyo kwa Mwananchi.

Elimu hii ya mpiga kura inatolewa na tume ilikuwafanya wananchi kushiriki katika chaguzi mbalimbali kuchagua au kuchaguliwa na kugombea katika jamii zao zinazowazunguka.

Tume ya Taifa ya uchaguzi imekuwa ikitumia wadau mbalimbali ilikufikisha ujumbe kwa wananchi ikiwemo Radio,Magazeti,Tv nawadau wengine wakaribu katika swala hili la ufikishaji Elimu ya uchaguzi kwa mpiga kura.
Kutokana na taarifa hizi za ujio wa Maskauti hao MAKALIBLOG, imepata nafasi ya kuzungumza na wakufunzi hao kutoka tume ya Taifa ya Uchaguzi baada ya kutua katika Radio moja mkoani Mara VICTORIA FM RADIO, ambapo sasa wameanza Rasimi kupeleka Elimu hii kwa wananchi katika wilaya zote za Mkoa wa Mara kupitia Radio hiyo ikiwa ni moja ya wadau.

Msafara huo ukiongozwa na watu watatu akiwamo Mkuu wa msafara ambapo pia wote ni watendaji watume ya taifa ya uchaguzi NEC. BW. SULEMANI BALULA, STEPHEN ELISANT, JOSEPH CHAROS.
Walisema kuwa kiini cha kuzunguka nchi nzima lengo nikuendana na kasi ya Uchumi wa ulimwengu kupata viongozi watakaoendana nakasi kupitia kwa wananchi viongozi wao watakao wachagua ama kunasababu ambazo ziliwafanya kutoelewa basi ninafasi ya kuelewa kupitia maskauti hawa.

Aidha wamesema kuwa matarajio ya Tume katika chaguzi zijazo nikupata viongozi walio bora waliochaguliwa na wananchi ambapo pia kupitia elimu hiii inayotolewa na tume nikuwafanya wanchi wasiwajutie viongozi walio wachagua na wala sikujuta.

     ''Tutaendelea kutoa elimu hii ilikuwafanya         wananchi waipate kwa uzuri ikiwa wataielewa vizuri basi watapiga kura vizuri tena kwa kujitoa wao wenyewe kwenda kupiga kura wao wenyewe bila kushurutishwa.''

Huku wakisema kuwa wataacha kutoa elimu hiii nisiku ya kupiga kura nasiku ya kutangaza matokeo ndio haitatolewa sababu ya sheria kutoruhusu lakini siku zingine zakawaida elimu hii itaendelewa kumfikia mwananchi kwa njia mbalimbali lengo nikupata viongoi bora.

MASKAUTI WAKIWA NDANI YA RADIO VICTORIA MUSOMA
Powered by Blogger.