MAAFISA WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI NEC WATUA MKOANI MARA KUFIKISHA ELIMU YA MPIGA KURA



MAAFISA WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI NEC WAKIWA KATIKA STUDIO ZA VICTORIA RADIO KUFIKISHA ELIMU YA MPIGA KURA MKOANI MARA KUSHOTO NI MKUU WA MSAFARA BW. SULEMANI BALULA KATIKATI NI BW.
STEPHEN ELISANTE NA KULIA N BW. JOSEPH CHAROS.


NA MAKALIBLOG; MUSOMA, MARA
Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC imefika Mkoani Mara kwa ajili ya kuendeleza zoezi la utoaji Elimu ya Mpiga kura ikiwa ni zoezi endelevu linalofanyika nchi nzima ili kufikisha Elimu ya Mpiga Kura ipasavyo kwa Mwananchi.

Elimu hii ya Mpiga Kura inatolewa na Tume ili kuwafanya wananchi waweze kuzifahamu taratibu za Uchaguzi ikiwemo za Uandikishaji wa Wapiga Kura na Hatua za Uchaguzi. Hii itapelekea wananchi wengi Zaidi kushiriki katika chaguzi mbalimbali kwa kuchagua au kuchaguliwa na kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi inatumia njia mbalimbali kufanikisha adhima yake ya kuhakikisha kuwa Elimu ya Mpiga Kura inawafikia wananchi wengi zaidi. Njia hizo ni pamoja na vyombo vya habari kama Radio, Magazeti, luninga na mitandao ya kijamii, Kutoa vibali vya kutoa elimu ya Mpiga kura kwa Taasisi na Asasi na Kufanya mikutano mbalimbali  na wadau.

Kutokana na taarifa za ujio wa Maafisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi MAKALIBLOG, imepata nafasi ya kuzungumza nao baada ya kutua katika kituo cha Radio cha VICTORIA FM kilichoko Mkoani Mara, ikiwa ni katika kutekeleza mkakati wao wa kuhakikisha wananchi wa Mara wanaelimishwa kwa kupitia Radio mbalimbali za Kijamii.

Maafisa hao ambao pia ni watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni BW. SULEMANI BALULA STEPHEN ELISANTE na JOSEPH CHAROS.

Katika maelezo yao walisema kuwa kiini cha Tume kuzunguka nchi nzima ni kutoa Elimu ya Mpiga Kura kwa lengo la kuwafanya wananchi wengi Zaidi waweze kutumia haki yao ya kikatiba ya Kuchagua au kuchaguliwa kama viongozi. Hii, itapelekea kupatikana kwa viongozi wanaoendana na kasi ya Uchumi wa ulimwengu.

Aidha, wamesema kuwa matarajio ya Tume katika chaguzi zijazo nikupata viongozi walio bora waliochaguliwa na wananchi ambapo pia kupitia elimu hii inayotolewa na Tume nikuwafanya wanchi wasiwajutie viongozi walio wachagua.



     ''Tutaendelea kutoa elimu hii ilikuwafanya  wananchi waipate kwa uzuri.  Ikiwa wataielewa vizuri basi watapiga kura vizuri tena kwa kujitoa wao wenyewe kwenda kupiga kura wao wenyewe bila kushurutishwa.''

Huku wakisema kuwa Elimu hii itatolewa katika kipindi chote cha mwaka tofauti na ilivyokuwa zamani isipokuwa kwa  siku ya Kupiga Kura na siku ya kutangaza matokeo kwani  sheria hairuhusu
Powered by Blogger.