HUSSEIN Machozi - Italy Hajulikani Alikiba Wala Diamond..!!! Burudani
Msanii wa muziki, Hussein Machozi, amefunguka kwa kudai kuwa hakuna
msanii wa muziki kutoka Tanzania ambaye anajulikana nchini Italy.
Aidha amedai muimbaji kutoka Kenya, Stella Mwangi ambaye anaishi nchini
Norway ndiye msanii wa Afrika Mashariki anayefanya vizuri.
Muimbaji huyo aliyewasili nchini Tanzania wiki hii akitokea Italy,
amedai nchini Italy muziki wa Tanzania haujafika na hata wasanii
wanaofanya vizuri nchini kwa sasa akiwemo Diamond na Alikiba
hawajulikani.
“Hapana lakini kuna mtu mmoja alishaniambia kuhusu msanii wa Kenya
anaitwa Stella Mwangi wanamfahamu fahamu, siyo kivile sana kutoka East
Africa,” alisema Hussein.
Aliongeza, “Bongo Fleva Italy sijawahi kuisikia kiukweli wa Mungu. Kama
kuna mshikaji mmoja nilimwambia kwetu kuna msanii mkali sana anaitwa
Diamond nikawa nimempa link akawa shabiki, akawapa na wengine wakawa
mashabiki wa Diamond kinyama.,”
Muimbaji huyo amedai amekuja nchini kwaajili ya kuachia kazi zake mpya
za muziki na baada ya hapo atarejea tena Italy kwaajili ya kuendelea na
masomo