MWENYEKITI WA CCM WILAYANI RORYA ASEMA HATA WASAMEHE WASIOFATA MADILI YA CHAMA
UNAWEZA KUTAZAMA MATUKIO YA PICHA MBALIMBALI YA MKUTANO HUO
Na MAKALIBLO.MARA
mwenyekiti wa ccm wilaya ya rorya SAMWELI KIBOYE,maarufu namba tatu kulia kwake ni katibu wa ccm mkoa wa mara.
Mwenyekiti wa ccm wilayani rorya samweli kiboye marufu namba tatu amesema hata wafumbia macho viongozi wowote watako kiuka maagizo ya chama katika chaguzi zozote kwa lengo lakulinda heshima ya chama.
Chama cha
mapinduzi (CCM) Mkoani Mara kimesema kuwa hakitafumbia macho kiongozi yeyote
atakayetumia Rushwa kwa lengo la kupata uongozi katika chaguzi zozote kwa lengo la kulinda heshima ya chama hicho
ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua kali kwa kutupilia mbali jina lake ili kupata
kiongozi mwenye sifa za kuongoza kwa
lengo la kuletea Watanzania Maendeleo.
Hayo
yamebainishwa na Katibu wa Chama hicho mkoani Mara Innocent Nanzabar Katika
kikao cha Halmashauri Kuu ya chama Wilayani
rorya Mkoani Mara
Naye
Mwenyekiti wa Chama cha Maapinduzi Wilayani rorya ameongeza kuwa katika
uchaguzi unaoendelea wa Mabalozi na Pamoja na Matawi hawatakubali kiongozi
ambaye hafuati maagizi kutoka ngazi za juu.
Robert
Manjebe Ni katibu wa wazazi mkoa wa Mara akazidi kusisitiza kwa wanachama hao
kufuata katiba ya Chama hicho.
Aidha Katibu
wa chama cha mapinduzi Wilayani rorya Mkoani Mara akisoma taarifa kwa
Mwenyekiti wa chama hicho anabainisha changamoto walizokumbana nazo katika
utendaji kazi.
wajumbe wakimfatilia mwenyekiti katika mkutano huo
samweli kiboye mwenyekiti wa ccm rorya almarufu namba tatu akizungumzakatika mkutano wa halamshauri kuu.
wajumbe wakiwa makini kabisa kufata kinachotelewa.