BABU WA MIAKA 71 AKAMATWA NA POLISI KWA KUMBAKA MJUKUU WAKE WA MIAKA 9
Kamanda wa polisi mkoani Pwani, kamishna msaidizi mwandamizi, Onesmo Lyanga, akizungumza na baadhi ya waandishi mkoani hapo.
****
MZEE Athuman Ramadhan Njuila ,miaka 71
,mkazi wa Mbwewe,Bagamoyo,mkoani Pwani anashikiliwa na jeshi la polisi,
kwa tuhuma ya kumbaka mtoto wa miaka 9, mwanafunzi wa darasa la pili
ambaye ni mjukuu wake.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari,Kamanda wa polisi mkoani Pwani, kamishna msaidizi mwandamizi, Onesmo Lyanga, alisema mzee
huyo alifanikuwa kufanya ukatili huo baada ya kumrubuni mtoto huyo
aingie ndani ya nyumba yake kusikiliza muungurumo wa mashine.
Alieleza kuwa baada ya mtoto huyo kuingia ndani,mtuhumiwa alimsukumia kitandani na kuanza kumwingilia kimwili.
"Baada ya kupata taarifa hizo, tarehe 24
Aprili mwaka huu,tulimhoji mama mzazi wa mtoto huyo ambaye alikiri
kutokea kwa tukio hilo "alieleza kamanda Lyanga.
Akisimulia mkasa huo,mtoto aliyefanyiwa
ukatili huo alisema siku hiyo alifika kwenye nyumba ya babu na kumkuta
akiwa na bibi yake baadaye bibi aliondoka na kumuacha akiwa na babu yake
ndipo babu akaanza kumwingilia kimwili.
Tayari jeshi la polisi limekamata mtuhumiwa Njuila kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.