MKUU WA MKOA WA MARA KUZUNGUMZA NA WAKANDARASI;
mkuu wa mkoa wa mara akizungumza na wanahabari mara baada ya ukaguzi wa barabara ya makutano juu sanzate yenye km 50 hivi karibuni.
sehemu ya ujenzi wa barabara ya makutano juu sanzate ukiendelea;
Mkuu
wa mkoa wa Mara Daktari Charles Mlingwa
ameigaiza ofisi ya Meneja wa Tanrods mkoa wa Mara kuwaita wakandarasi
wazalendo wote mkoani hapa kukutana kujadili utendaji wao.
Agizo hilo limekuja wakati mkuu wa mkoa wa Mara
akifanya ukaguzi wa ujenzi na ukarabati wa barabara ya Mika Utegi Shirati
kujengwa chini ya kiwango.
Mkuu wa mkoa huyo alisema lengo la kuwaita ni kuwafahamisha jinsi serikali inavyotaka kazi
inanywe baada ya kutoridhishwa na kasi ya ujenzi na ukarabati wa barabara ya
lami nyepesi ya Mika -Utegi
yenye urefu wa kilomita 8 inayogharimu sh 852 milioni.
“Na kuagiza uwaite haraka iwezekanavyo wakandarasi
wote wanaohusika na ujenzi wa barabara zetu ili tuwafahamishe jinsi serikali
inavyofanyakazi zake kwani kasi wanayoenda nayo haikidhi viwango tunavyotaka,”
alisema Mlingwa.
Mlingwa alisema kuwa anataka kuwasikiliza
wakandarasi wazawa ili kufahamu changamoto wanazokutana nazo jinsi wanayofanya
kazi na kile serikali inavyotakiwa kufanyika na wafanye kwa kasi na kwa viwango
vinavyotakiwa.
“Kikao hiki kifanyike mapema mwezi wa tano kazi ya
utengenezaji wa kipande hiki hauniridhishi na uko chini sana ya kiwango, kwa
sababu ni kweli tuwe na wakandarasi wazawa lakini pia kitumike kama sehemu ya
kufahamiana, kwani
Kwa upande wake Meneja wa Tanroads mkoani Mara Mhandisi
Mlima Felix aliwataka wananchi kutokujenga kando ya barabara ili badaye walipwe
na serikali (tegesha) ambapo watakuwa
wanajidanganya na kupoteza muda wao ya kwamba watapata fidia.
“Tunachangamoto ya kukabiliana na wananchi kujenga kandokando na hifadhi ya barabara kwa lengo la kutegesha ili waje walipwe tunaomba serikali kuliangalia hili kwani limekwamisha ujenzi wa miradi ya barabara katika mkoa wa mara kukwama na kushindwa kukabidhiwa kwa wakati,”alisema Felix.