MIAKA 60 JELA KWA KOSA LA UNYANG'ANYI KWA KUTUMIA SILAHA
Na Eva-Sweet Musiba
MUSOMA- MARA
WATU wawili
Jumanne Wambura(34) na Bkobe Bhoke(30) wakazi wa kijiji cha Pida Wilaya ya
Butiama Mkoa wa Mara wamehumiwa kwenda jela kila mmoja miaka 30 kwa kosa la
unyang’anyi kwa kutumia silaha
kinyume na kifungu cha sheria namba 287 A kanuni ya adhabu iliyofanyiwa mapitio mwaka 2002 na
mapitio tena na sheria namba 3 ya mwaka 2011.
Akitoa
hukumu hiyo, jana,hakimu mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Musoma,
Kharimu
Mushi alisema kutokana na ushahidi wa
shahidi wa kwanza ambaye Mahakama ilimwona hana vidole na wa pili, Mahakama hiyo imeona itoe adhabu
hiyo ili iwe fundisho kwa wengine na baada ya kifungo hicho watalipa Sh Milioni
2 kila mmoja kama sehemu ya malipo kwa majeraha aliyoyapata.
Alisema kuwa
watu hao walitenda kosa hilo, septemba 29 mwaka 2014 na
baada ya kumkata kwa panga vidole
vitatu na kukatika walichukua Shilingi Milioni 1,200,000 mali ya Matiku Mwita.
Waendesha
mashitaka walileta ushahidi wao, katika ushahidi, shahidi wa kwanza, Matiku
Mwita(34) aliielezea Mahakama kuwa majira ya siku 6 za usiku katika eneo la
Pida akiwa nyumbani kwake aliona watu sita aliwatambua hao ambapo mshitakiwa wa
pili alivunja taa lakini tayari alikuwa amemwona na kufanikiwa kuingia ndani na ndipo
alipokatwa vidole vitatu vya mkono wa kushoto.
Aliendelea kwa
kusema kuwa baada ya kumkata vidole vyake kwa maumivu makali aliyokuwa nayo
alimwambia mkewe zilipo pesa ili atoe awapatie ili kunusuru roho yake,ambapo
aliwatupia fedha hizo kwa kuwatupia
dirishani.
Naye shahidi
wa pili Magreth Matiku aliiambia mahakama kuwa siku ya tukio aliona watu nje
wakiwa na mapanga na marungu, walivunja mlango na kuingia ndani ambapo
walimkata kwa panga mumewe mkono wa
kushoto na kuvuja damu nyingi na alitoa fedha ili kunusuru roho ya mumewe kwa
kuzitupa nje kupitia dirishani na aliweza kuwatambua hao kwa kuwa nje kuna taa
ya umeme wa jua (solar Power).
Naye
mwendesha mashitaka, wakili wa serikali Frank Nchanila aliimbia Mahakama kuwa
kwa kuzingatia kosa la unyang’anyi kwa kutumia silaha, vinaleta kifo na tayari
Matiku Mwita ni mlemavu anaiomba Mahakama itoe adhabu kali ili iwe fundisho kwa
wengine.
Katika
utetezi wao, mshitakiwa wa kwanza
aliiomba Mahakama kumpunguzia
adhabukwa kuwa amefanyiwa upasuaji ambapo wa pili alidai kuwa ana
familia, mke na watoto sita na kwamba Mama yake Mzazi ni mlemavu na ana
tatizo la bandama ambapo pia aliomba nakala ya hukumu.
Mashahidi
wengine katika kesi hiyo walikuwa mpelelezi wa kesi hiyo,G 8299 PC Adam, Nyori
Mwita na John Magesa.
MWISHO.