KIGERA FC WATISHIA KUGOMEA MASHINDANO YA ABU TEGE ENDAPO TIMU YA JESHI LAKUTULIZA GHASIA F.FU MUSOMA WATASHIRIKI;



 
Mashabiki wa mpira wa miguu wa timu ya kigera fc wamewaomba wachezaji wa timu hiyo kutoyagomea mashindano ya ABU TEGE CONCIOUS NDONDO CUP
ambayo yalianza kutimua vumbi katika viwanaja vya mara secondary  na kuvunjika kutokana timu ya F.F U, musoma kufanya fujo katika mashindano hayo.
Tarifa za kuaminika kutoka katika clabu ya kigera fc almarufu maveterani zinadai kuwa hawataweza kushiriki katika mashindano hayo kutokana na fujo zilizofanywa na timu hiyo ya jeshi la kutuliza ghasia katika mchezo uliochewa march5,2017, siiku ya jumapili endapo polisi wakishiriki basi maveterani hawatashiriki tena.
Katika mchezo huo uliokuwa chini ya referee bw, mwinyi kutoka musoma ambapo hadi dakika ya sabini na tano kigera walikuwa wakiongoza kwa magoli manne kwa mawaili.
Wameahidi kutoshiriki mashindano hayo kutokana na vurugu ambazo zinaweza kujitokeza katika mashindano hayo ambao baadhi ya askari poli wanaochezea katika kikosi hicho nawasio wachezaji wamekuwa na tabia ya kuanzisha fujo timu yao inapokuwa inafungwa.
      “”Manjua atakuja kuumia mtu hapa tulete fujo wao wamekuwa wakifungwa wanagomea iweje sisi tukikutana nao robo fainali au nusu fainali watufunge unafikiri mashabiki wetu watatuelewa hawawei wataanzisha fujo ilikulipiza kisasi,Alisema mmoja wawachezaji wa kigera vetelani.
Ambapo inadaiwa watu kazaa waliumizwa kwa kupigwa na maskari polisi hao kutokana nakuanza kuwashambulia wananchi ,mmoja waliojeruhiwa ni mwanajeshi wa jeshi la wananchi Tanzania aliezingirwa nakuanza kushambuliwa na askar polis hao pamoja na raia wengine ambao mpaka sasa ni majeruhi kwakupigwa na maaskari hao.
Mpaka sasa kuna baadhi ya mashabiki ambao wamepanga kuwafungulia kesi baadhi ya maaskari polisi walioshiriki katika kitendo hicho ilikupata haki yao ya msingi mpaka sasa polisi hao wamejenga uhasama na baadhi ya raia kutokana na kushindwa kutumia mchezo kama njia rahisi ya kuwaunganisha raia na polisi.
Ikumbukwe kuwa simara ya kwanza wachezaji wa timu hiyo kufanya fujo kwani December,2016 mashindano yaliyo fanyika katika viwanja hivyo hivyo waligomea penart na hatimae kuanzisha fujo katika mashindano na timu hiyo ya polisi kuondolewa kwa mujibu wakanuni ya mashindano hayo.
   “Tutaleta matatio wakirudi hawa kwani wametutishia kutukamata kwa kutufata hadi nyumbani iweje waje wacheze tena nibora tujiondoe sisi ilikutoa fujo ambazo zinaweza kuibuka’ alisema mmoja wachezaji wa kigera fc.
Kigera fc ama maveteran ni mmoja ya timu kubwa na yenye washabiki wengi mfano wa samba au yanga za dare s salam ambapo nanimoja ya timu yenye historia ya kutofungwa kirahisi katika viwanja vya nyumabi ambapo timu nyingi zimekuwa zikipata tabu sana kuifunga timu hiyo ambapo mmoja kubwa ni polis force ya musoma ambapo wamekuwa wakianzisha fujo kila wanapokutana na timu hiyo.
Na maliza na kusema lazima askari hawa waangaliwe kwani wao nichachu ya kujenga ukaribu na raia nasikujenga uadui ambapo hiii inaweza kusababisha kutopata tarifa ama ushirikiano wakati wakitimiza shughuiza zao salamu kwa bodi ya michezo mkoa wa mara kuangalia timu zinazoshiriki nakuzipa kipaumbele ilikuoko vijana wanao tafuta ulaji kupitia gozi la ng’ombe
Powered by Blogger.