Wema Sepetu Kaachiwa Huru Kwa Dhamana ya Sh. Milioni 5

Msanii wa filamu  nchini na Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu, mchana huu  amepandishwa kizimbani kwenye mahamaka ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

Akisomewa mashtaka na wakili wa serikali Nassoro Katuga mbele ya Hakimu Mkazi Thomas Simba imeelezwa kuwa msanii huyo alikutwa na kiwango kidogo cha dwa za kulevya aina ya bangi 

Wakili Nassoro Katuga amesema mahakamani hapo kuwa mtuhumiwa Wema Sepetu mnamo tarehe 4 mwezi wa pili mwaka 2017 katika eneo la Kunduchi Ununio watuhumiwa watatu akiwemo Wema Sepetu walitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha sheria ya kuzuia na kupambana na dawa ya kulevya kifungu cha 17 (1) (a) cha makosa hayo.

Msanii huyo na wenzake wameachiwa kwa dhamana ya shilingi milioni 5 na wadhamini wawili na kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe 22 Februari 2017 itakapotajwa tena na kwamba bado uchunguzi unaendelea
.
Powered by Blogger.