TUNDA MAN ADAI KUPOKEA SIMU NYINGI KUHUSIAN NA JINA LAKE KUTAJWA KWENYE MTANDAO WA MADAWA YA KULEVYA;
Msanii
wa muziki Tunda Man amedai jana alipokea simu nyingi baada ya Mkuu wa
mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kutangaza list mpya ya majina ya watu
wanaotuhumiwa kujihusisha na biashara ya Madawa ya kulevya ilikiwemo
jina la Tunda ambaye ni video queen.
Baadhi
ya waandishi kwenye mitandao ya kijamii waliandika jina Tunda bila
kutolea ufafanuzi ni Tunda gani, hali ambayo iliwafanya wasiohusika
kupigiwa simu nyingi akiwemo msanii wa muziki Tunda Man.
Tunda Man amedai wengi ambao ulikuwa wanampigia simu walitaka kujua kama kweli ni yeye ndiye aliyetajwa au ni Tunda mwingine.
“Jaman
Tunda alietajwa na Mh Paul Makonda ni huyu sio mie maaana simu zimekuwa
nyingi @soudybrown na wewe hujui au umeamua tu kunipigia,” aliandika Tunda Man Instagram huku akiwa amempost dada huyo.
Pia kwenye list hiyo mpya alitajwa mwanadada Vanessa Mdee ambaye pia anatakiwa kuripoti makao makuu polisi Jumatatu.
NA MPE BLOG