CCM Yabadili Gia Angani
Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amesema chama hicho siku
ya kesho tarehe 5 mwezi wa pili kitakuwa kikitimiza miaka 40 toka
kimezaliwa, kimefanya mabadiliko katika kusherehekea siku hiyo kwa
kufanya shughuli mbalimbali za kijamii
Polepole
amesema toka chama hicho kimeanzishwa kimekuwa ni chama cha wananchama
na chama ambacho kinashughulika na masuala ya watu watu pamoja na
matatizo yao, hivyo mwaka huu wameamua kusherehekea
siku hiyo kwa namna tofauti kwani hawatukuwa na sherehe kama desturi
yao bali watasherehekea kwa kushiriki shuguli za kijamii.
"Maadhimisho
ya mwaka huu yatakuwa tofauti kidesturi kama ambavyo yamefanyika hapo
mwanzoni hivyo hatutakuwa na sherehe kama ilivyodesturi ya mikutano
mikubwa ya hadhara , kwa maana ya uzinduzi na kilele isipokuwa mwaka huu
tutafanya shughuli za maadhimisho ya CCM kwa namna kuu mbili, moja ni
kwa kushiriki shughuli za kijamii, shughuli ambazo moja kwa moja
zinagusa maisha ya watu wetu, jambo la pili ni mikutano ya ndani na hapa
wanachama wote wa CCM watashiriki mikutano ya ndani kuanzia mikoa,
ngazi ya wilaya, ngazi za majimbo, ngazi za kata na ngazi za matawi kwa
kushirikisha mashina yetu kote nchini Tanzania."
Mbali
na hilo Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amesema
kuwa maadhimisho ya miaka 40 ya CCM kwa mwaka huu yatafanyika kwa mwaka
mzima huu wa 2017.
Ikumbukwe
kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kilizaliwa tarehe 5 Februari, 1977
kutokana na kuvunjwa kwa vyama vya Tanganyika African National Union
(TANU) na Afro-Shirazi Party (ASP).