Kutana na Mzee wa miaka 74 aliejiunga FORM ONE na Wanawe wawili
Mzee mwenyewe kwenye hii habari anaitwa Kazungu Humadi Kadenge na umri wake ni miaka 74 na anatokea kijiji cha Kimbule Ganze Kilifi Kenya ambapo aliamua kurudi Shule ili kuepuka kuitwa mchawi sababu hajui kusoma wala kuandika.
Iliripotiwa kwamba Kadenge alijiunga rasmi na kidato cha kwanza katika shule ya Ganze Boys Secondary School na kwa juhudi zake alipata alama 134 mwaka jana katika cheti cha elimu ya msingi (KCPE) katika shule ya msingi Ganze, Kenya ambapo kwenye shule hiyo anasoma pamoja na watoto wake wawili wa kiume.
Mtu mwingne anayeshikilia rekodi ya kusoma uzeeni Kenya ni marehemu Kimani Maruge ambaye aliingizwa kwenye kitabu cha rekodi za dunia cha Guinness kwa kuwa mtu mkongwe kuanza shule ya msingi, alijiunga na darasa la kwanza Januari 12, 2004 akiwa na umri wa miaka 84.