NA MAKALI BLOG
Rorya.
Askofu mkuu wa kanisa la
Waadventista Wasabato konferensi ya Mara, George Ojwang' amewaagiza
wachungaji wa mitaa, na wazee wa makanisa kuwashughulikia waumini wao
wanaojihusisha na ulimaji na uuzaji wa madawa ya kulevya.
Kingozi huyo aliyasema hayo jana
katika sherehe za kumsimika mchungaji mpya wa mtaa wa Mauwe ulioko kata
ya Kitembe Wilayani Rorya aliyechukua nafasi ya mtangulizi wake Dawa Ochupe.
Ojwang' aliagiza viongozi hao
kuwachulia hata za kinidhamu kulingana na kanuni na miongozo ya hilo ikiwa ni
njia ya kulilinda na mmomonyoko wa maadili yanayoendelea nchini.
"Hatuwezi kuendelea kulea
watu wanaopingana na miongozo ya kanisa na kuvunjwa kanuni za kanisa
zinazotuongoza, viongozi wote nawagiza washughulikieni waumini wanaojihusisha
na biashara ama kilimo cha madawa ya kulevya," alisema Askofu Jana.
Aliongeza kuwa ikiwa kanisa
litakuwa safi hata serikali haitakuwa na muda wa kushughulikia watu kama hawa
ambao wanasababisha nguvu kazi ya taifa kupotea huku wengine wakipata mapato
ya udhalimu jambo ambapo hata vitabu vitakatifu vinakataa.
Diwani wa kata ya Kitembe Thomas
Risa (CHADEMA) alisema katika kata yake vita hiyo alianza mapema tamgu
alipoingia kwenye udiwani kwani alijua madhara yake kwa wa kazi wa kata ya
kitembe.
"Hata unywaji wa pombe kupita
kiasi ushughulikiwe kama ilivyo kwenye madawa ya kulevya ili kuwafanya vijana
wanaotumia muda mwingi kutafuta madawa na pombe wautumie kwenye kufanya kazi
za uzalishaji Mali," alisema Risa.
Aidha Risa aliipongeza serikali
kupitia jeshi LA polisi kwa kushirikiana naye picha ya kuwa diwani wa Chadema
katika kupiga vita madawa ya kulevya katika kata yake.
"Nilianza kupambana na watu
hawa yangu nilipoingia kwenye nafasi ya uongozi wa udiwani, na mwananchi
wangu wameniunga mkono hivyo tumepata mafanikio makubwa katika kupiga vita
suala hili," alisema Risa.
|