AUA KAKA YAKE KWA KUCHELEWA KUPIKA
Tarime.
Mkazi wa
kitongoji cha Bondeni, kijiji cha Mpakani katika mji mdogo wa Sirari
Nandi Lula (19) anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kumchoma kisu
kaka yake, Masuke Lula (25) na kumsababishia kifo kutokana na kuvuja damu
nyingi.
Kamanda wa mkoa wa Polisi,Tarime/Rorya Andrew Satta
amesema tukio hili lilitokea usiku wa Januari 30 kwa marehemu aliemtaja kuwa ni
Masuke Lula (25) aliyeanzisha ugomvi kwa mgodo wake Nandi Lula (19) kwa
kuchelewa kuandaa chakula na kuanza kumgombeza.
Aliongeza kuwa jamii inapaswa kuwa makini na kutumia
busara ili kuepusha madhara na vifo vizivyo tarajiwa kama hiki ambacho
kilitokana na kumgombeza mdogo wake hivyo kumsabaishia apandwe hasira na kumuua
kaka yake.
“Alifariki palepale kwenye tukio baada ya kuchomwa
visu mdomoni, na mgongoni na kumasbabishia mauti,”alisema Kamanda Satta.
Shuhuda wa tukio hilo,Willison Patrick alisema baada
ya marehemu kufika nyumbani huku amelewa alimkuta mdogo wake akikatakata nyanya
kwa ajili ya kupika mboga na kuanza kumgombeza ambo ambalo lilichochea hasira
kwa mdogo wke.
“Alimpiga makofi mdogo wake, ndipo mtuhumiwa
akakasirika na kutumia kisu alichokuwa akikatia nyanya na kumchoma mdomoni na
mgongoni akafia palepale,”alisema Patrick.
Mhudumu wa chumba cha kuhifadhia maiti katika
Hospitali ya Mji wa Tarime, Samwel Malindi alikiri kuupokea mwili wa marehemu
na kuwa umehifadhiwa kwa ajili ya kusubiri taratibu za maziko zifanywe na ndugu
wa marehemu.