BIASHARA UNITED HAOO WAINUSA LIGI KUU WAITADIKA ALLIANCE YA MWANZA 2-0



Biashara united mara wamejikita kileleni mwakundi  C wakiwa na pointi 23  baada ya kuibuka na ushindi mwingine mnono wa mabao 2 kwa bila katika ligi daraja la kwanza dhidi ya alliance ya mwanza mchezo ambao ulipigwa katika uwanja wa karume mjini musoma mkoani mara.

Biashara iliwachukua dakika ya 31 mwakipindi cha kwanza kuandika bao kupitia kwa mchezaji wa Yule Yule aliyewalaza pamba Songa Jeradi nkuitanguliza mbele Biashara united mara, hadi kipyenga cha mwamuzi kuelekea mapumziko Biashara united Mara walikuwa wakiongoza kwa bao 1.

Kpindi cha pili kilianza kila timu ikitafuta bao huku Alliance wakitafuta kusawazisha biashara wao walikuwa wakitafuta kuongeza boa jingine ambapo iliwachukua hadi dakika ya 82 kupitia kwa mchezaji Nasoro Idd nakuiandikia Biashara Bao la 2 ambapo mpaka dakika 90 Biashara 2 alliance hawakupata kitu.

Tukazungumza na mwalim wa timu ya alliance mbwana makata ambapo alikili kuwa mchezo ulikuwa mzuri na ambao ulichezeshwa vizuri hivyo alikubaliana na matokeo ya mchezo huku akijipanga kupambana kwa michezo iliyobaki ilikuji hakikishia nafasi ya kucheza ligi kuu msimu ujao.

Naye kwa upande wake msimamizi kutoa shirikisho la soka tanzani TFF Jemedai Saidi alisema kila timu inahitaji kupanda daraja hivyo aliwapongeza wamzi wamchezo huo kutokana na kumuudu nakuchezesha kwa hali na kiwango cha juu huku mabao yaliyofungwa na Biashara alisema ni magoli yaliyofungwa kihalali.

“Niseme kwamba mabao yote yaliyofungwa nimagoli yakiufundi hivyo ndio tulitarajia katika mchezo maana timu hizi kila timu inatafuta kucheza ligi kuu msimu ujao hivyo tunashukuru mchezo umeisha vyema nahakuna shutuma zozote nahivyo ndio tunahitaji”alisema saidi.

Aidha nijambo la kupongezwa kwa timu ya biashara kwani sasa naiona ile kiu ya miaka mingi kuchezwa ligi kuu mkoani mara inaelekea kuisha sote tuipongeze na kuwashauri michezo iliyobaki washinde natuendelee kujipongeza.
Powered by Blogger.