MVUA ZILIZOANZA KUNYESHA MKOA WA MARA ZALETA MADHARA KWA WANANCHI NA TAASISI
sipicha hali ya tukio
Rorya.
Rorya.
Wakati mvua zinazoanza kunyesha nchini zikiwa
ni za kwanza baada ya kipindi kirefu za cha kiangazi, zimeambatana na upepo
mkali na kusababisha maafa katika shule ya sekondari Kisumwa nashule ya Msingi
Nyancha kuezuliwa na baadhi ya majengo kubomoka.
Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Simion Chacha ambaye pia ni
mwenyekiti wa maafa Wilayani hapa amesema kuwa katika shule ya sekondari
Kisumwa majengo mawili ya maabara yameezuliwa na kuabomoka huku, chumba kimoja
cha darasa kikibomoka kutaokana na upepo huo.
Amesema kuwa tukio hilo lilitokea januari 28 wakati
ambapo hakuna wananfunzi shule kwa kuwa ilikuwa siku ya mwisho wa wiki ambapo
hata hivyo serikali imeagiza idara husika kufanya tahithini za uhalibifu
uliofanyika katika shule hizo.
“Tumefika pale na mkurugenzi tukaona mvua
iliyonyesha jana (juzi) ikiambatana na upepo iliezua maabara moja, chumba
kimoja cha darasa, choo, tumewakatuta bodi ya shule na kupeana na maagizo kuwa
kesho (Jana) yaanze kukarabatiwa,” alisema DC Chacha.
Alisema kuwa mkurugenzi na wataalamu wake wataanza
kufanya ukarabati ule mdogo ili kuwapa nafasi wananfunzi waenelee kusoma,
lakini jengo la maabara litafanyiwa upembuzi wa kutosha na kujengwa upya kwani
liliharibika vibaya.
Hata hivyo mkuu huyo wa Wilaya alisema bado
tathimini ya uharibifu haijafahamika ili kufahamu kwa uhalisia wa hasara
iliyosababishwa na na mvua hiyo ya upepo.
Diwani wa kata ya Kisumwa Mwita Malawa amewataka
wananchi kuchangia nguvu kazi katika kurejesha hali nzuri ya majengo hayo kwa
kuwafanya wanafunzi hasa madarasa yenye mitihani kupata sehemu ya kusomea na
kujiandaa na mitihani yao.
Kwa upande wake mwananfunzi wa kidato cha nne Nice
Joshua alisema ikiwa vyuma vya maabara havitakamilika kwa haraka huenda
wakashindwa kufanya vizuri masomo ya vitendo.
“Tumeathirika kisaikolojia kwani sisi tuko kidato
cha nne na tunategemea kufanya majaribio mengi ya kisayansi ili kuweza kufanya
vizuri kwenye mitihani yetu inayohitaji vitendo,”alisema Joshua.
Kwa upande wake mkuu wa shule hiyo, Joshua John
alisema hakuna madhara zaidi yaliyotokea kwa wananfunzi wanaoishi hapo shuleni
kwani mabweni yao hayakuguswa na tufani hiyo
MAKALI NEWZ BLOG
MAKALI NEWZ BLOG