ANGALIA..PROFESA MUHONGO ALIVYOZINDUA UJENZI WA KITUO CHA AFYA NYAMBONO



Mbunge Profesa muhongo akizindua uwekaji wa jiwe la msingi katika kituo cha afya nyambono kushoto ni mratibu wa ujenzi wa kituo cha afya Bwana Majura Songo


Mratibu wa mradi wa ujenzi wa kituo cha afya Nyambono Dkt. Majura Songo (kushoto) akisoma taarifa ya mradi huo. Kulia ni mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Prof. Sospeter Muhongo ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye hafla hiyo, akifuatilia kwa makini taarifa hiyo.

kushoto ni mratibu wa mradi wa ujenzi wakituo cha afya Nyambono Bw. majura songo (katikati) ni profesa muhongo akipokea maelekezo kutoka kwa mratibu wa mradi, kulia aliyevalia tshert ni DR .Bwire Chilangi
Profesa muhongo akizunguka kuangalia eneo ambapo inajengwa kituo cha zahanati nyambono





sehemu ya wananchi walijitokeza katika hafla hiyo
MAKALIBLOG. MARA
Wananchi katika kata ya nyambono halmashauri ya musoma baada ya kuteseka kwa mda mrefu kwakukosa huduma za afya katika kijiji hicho hatimaye wamejitolea maeneo yao kwa ajiri ya ujenzi wa kituo cha afya kwa ajili ya kuokoa maisha yao.


Ujenzi wa kituo hicho umezinduliwa na Mbunge wa jimbo la musoma vijijini Profesa sospeter muhongo ambapo aliweka jiwe la msingi kuashiria kuanza ujenzi wa kituo hicho.


Profesa mhongo aliwataka wananchi kujitoa kwa ajiri ya maenendeleo ya kijiji hicho hivyo nivyema wakaungana ili kukamilisha kituo hicho nakuokoa maisha ya wananchi ambao yamekuwa yakipotea kwakukosa huduma za afya.


Mbunge huyo aliwataka wananchi kuhakikisha wanakamilisha ujenzi waukuta huku yeye akiahidi kupaua jengo ambalo litakuwa limekamilika kujengwa.

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Prof. Sospeter Muhongo aliwashukuru wananchi wa kijiji cha Nyambono kwa kubuni mradi huo mzuri na ameahidi kuchangia shughuli nzima ya uezekaji wa majengo hayo mara tu yatakapokuwa yamekamilika ujenzi wake.


“Mim naahidi endapo mkimaliza kujenga msaada wangu itakuwa ni kupaua jengo hilo lote huo ndio itakuwa msaada wangu kwahiyo ninyi nikujituma sasa kukamilisha ujenzi wa world hiyo”alisema profesa muhongo.

Akitoa taarifa mratibu wa ujenzi wa kituo hicho cha afya nyambono, Bwana Majura songo alisema Mradi wa Ujenzi wa kituo hicho ukikamilika kama ulivyopangwa utasaidia wananchi zaidi ya elf tano huku mradi huo ukitarajiwa kukamilika mwaka 2018.


Mradi huo unagaharibu kiasi cha shilingi Bilioni 2.2 ambapo yatakuwepo majengo 12 vyumba 3 vya madaktari huku world 28 huku michango zaidi ya ujenzi wa kituo hicho ikitegemewe kutoka kwa wadau na wazawa wa kijiji hicho ambao wanafanya kazi nje ya mkoa wa mara na walio ndani ya mkoa.

Dkt. Songo alisisitiza kuwa, mradi wa ujenzi wa kituo cha afya ni shirikishi ambapo unawahusisha wananchi wa kijiji cha Nyambono walioko ndani na nje ya kijiji, marafiki, viongozi wote wa Musoma vijijini na Halmashauri ya wilaya ya Musoma, huku wananchi wanashiriki nguvu kazi kama vile kusomba mawe, mchanga na mafundi, wananchi waishio nje ya Nyambono wanashiriki kutoa michango ya saruji 350 ambayo tayari imepatikana mifuko 69 na zoezi bado linaendelea.


“Ndugu mgeni rasmi, mradi huu ni shirikishi ambapo unajumuisha wananchi walioko nje na ndani ya kijiji cha Nyambono, viongozi wa kata na kijiji pamoja na Halmashauri ya wilaya ya Musoma” alieleza Dkt. Songo.


Hata hivyo, kituo cha Nyambono kimekadiriwa kugharimu shilingi za kitanzania bilioni 2.2 na kitakuwa na jumla ya majengo 12 likiwemo jengo la OPD ambalo tayari ujenzi wake umeanza kutekelezwa, jengo la mama na mtoto na majengo mengine yote kulingana na muongozo kamili wa ujenzi unaostahili kwa mujibu wa taratibu.


Nao kwa upande wao wakina mama wa kijiji hicho akiwemo Elizabeth misango yeye alisema kukamilika kwa kituo hicho ni asilimia kubwa sasa wananchi watakuwa wanapata hudma sitahiki nakuokoa maisha yao kwa umbali waliokuwa wakitembea .

Hafla hiyo ya uwekaji wa jiwe la Msingi ilienda sambamba na sherehe za sikukuu ya Krismasi ambapo Prof. Muhongo aliungana na marafiki zake Dkt. Christa na Wolf kutoka Ujerumani walioungana na wananchi wa jimbo lake kuazimisha sikukuu hiyo kwa kushiriki chakula cha pamoja na wananchi wake.
Awali mbunge wa jimbo hilo alishiriki katika ibaada ya krismas katika kanisa la menonight kivulini Tanzania (KMKT) lililopo katika tarafa Nyanja katika halmashauri ya musoma.


                 MAONI YAKO WEKA HAPO CHINI MATUSI

                                    (HAPANA)


                       HABARI NA MATUKIO 'TUPIGIE KWA 0754295996

                     AU Tutumie maoni yako kwa mussaj970@gmail.com
Powered by Blogger.