WALIMU WAISHI KWENYE MADARASA TARIME

Baadhi ya walimu wanaofundisha katika shule ya msingi Nyamwigula iliyoko kata ya Binagi Wilayani Tarime mkoani Mara wanaishi kwenye vyumba vya madarasa kutokana na nyumbza zao walizokuwa wakiishi hapo awali kuezuliwa na upepo
ulioambatana na mvua zilizanza kunyesha nchini.
Mwalimu mkuu shule ya Msingi Nyamwigula Otieno Magori amesema wanalazimika kutumia darasa kama ofisi na nyumba za kuishi kwa sababu mwaka jana maafa kama hayo yaliikumba shule hiyo na kuezua vyumba vinne vya madarasa na ofisi moja ya walimu ambavyo  mpaka sasa havijakamilika na ujenzi unaendelea.
Diwani  wa kata ya Binagi Mwarwa Chacha Maligili  ameiomba serikali na wadau wa elimu ambao wamesoma katika shule hiyo kujitokeza kuchangia ili kujenga na kumalizia maboma yaliyopo  kuwanusuru wanafunzi ambao sasa wanakaa kwa kubanana kwani mvua zilizoanza kunyesha hata majengo yaliyobaki siyo rafiki.
Mwenyekiti wa kijiji cha Nyamwigula Paul Magele na Mrimi Malisa ambaye ni  Mwenyekiti wa kamati ya Maendeleo wamesema tayari wameweka  jitihada za kutatua changamoto hiyo na kuwa ni kuwashirikisha wananchi kwa kuchangia licha ya kuwa kuna hali mbali ya kiuchumi ili kuhakikisha kuwa wamefanikiwa kuimarisha majengo hayo kwa kuyajenga upya.
Hata hivyo  baadhi ya Wananchi wamedai kuwa, mbali na shule hiyo kukumbwa na maafa, bado mashamba yao yameharibika kutokana na mvua  iliyoambatana na upepo mkali na kuangusha migomba ambayo walikuwa wakiitegemea kwa chakula baaada ya kuwepo kwa kiangazi na ukame wa Muda mrefu na kusababisha mazao waliyokuwa wamepanda kukauka.
Powered by Blogger.