Wakazi wa Arusha wapata ahueni ya majanga ya mvua kwa kuwekewa daraja katika Mto Kijenge
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Mashaka Gambo amefanya uzzindua daraja la Mto
Kijenge linalounganisha kata za Engutoto na Moshono ambalo limejengwa
kwa ufadhili wa Kampuni ya Dharam Singh Hanspaul.
Akizungumza
katika uzinduzi huo Mkuu wa Mkoa amesema daraja hilo ni ukombozi na
msaada kwa wananchi wengi ambao walikua wakipata adha kubwa ya kuvuka
haswa wakati wa mvua kutokana na kukosa kivuko cha uhakika na kivuko
kilichokuwepo awali kiliashiria hali ya hatari kubwa kwa watoto, wazee,
waendesha pikipiki, waenda kwa miguu wote na zaidi hakuna Gari
lililokuwa na uwezo wa kupita hapo.
Hii
ndio tunayoita kurudisha kwa jamii “Community Social Responsibility”,
kampuni hii ya Hanspaul imetoa msaada ambao utatoa mchango mkubwa sana
kwa jamii na sisi kama Serikali tunafarijika kwa kuona wadau wanaunga
mkono jitihada za Serikaili kwa kiwango hiki hili ni jambo la kuigwa na
Kampuni nyingine wajifunze katika hili.
Katika
uzinduzi wa daraja hili Gambo alitumia fursa hiyo alisikiliza kero za
wananchi waliohudhuria na ambao wamelalamikia uuzaji holela wa maeneo ya
wazi ya Serikali hali inayopelekea uhaba wa maeneo ya kujenga huduma za
kijamii kama zahanati na shule huduma ambazo hazipatikani katika kata
ya Engutoto hiyo hivyo wameiomba serikali itatue tatizo hilo ili
wananchi wapate huduma bora za ijamii.
Akiwasilisha
kero zake mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Bi. Zaituni Marunda amesema
kuwa licha ya uuzaji holela wa ardhi kuna migogoro ya ardhi katika kata
hiyo na wananchi wengi wanaomiliki ardhi bado hajapatiwa hati jambo
ambalo linawapa wasiwasi kuwa huenda ardhi zao zikamegwa na wawekezaji.
Aidha
Neema John aliongeza kuwa kwa kipindi kirefu katika maeneo hayo
wamekuwa wakisumbuliwa na kero za maji, umeme na Zahanati hivyo
wameiomba Serikali iwasaidie kutatua kero hizo znazowaathiri zaidi
kinamama ambao hutembea umbali mrefu wakitafuta huduma za maji pamoja na
kupata taabu wakati wa kujifungua.
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ameagiza ofisi ya Mkurugenzi kumkabidhi
ripoti ya maeneo ya wazi ya jiji yaliyouzwa kienyeji ili aweze
kushughulikia kero na pia aliweza kuhamasisha ujenzi wa Zahanati ya Kata
kwa kuchangia Bati 100 na kuungwa mkono na Bw. Hans Paul aliyetoa
matofali 5000 huku Bw. Jagjit Aggarwal akichangia mifuko ya saruji 200
na Mkurugenzi wa Jiji Bw. Athumani Kihamia kuahudi kukamilisha ujenzi wa
zahanati hiyo.
Daraja
la Mto kijenge lilioanza kujengwa mwezi Juni na kukamilika Agost 2016
lina upana wa Mita 20, uwezo wa kupitisha magari yenye uzito wa Tani
tatu(3), urefu kwenda juu ni mita 2.2, uimara wa pekee na linaweza
kudumu kwa miaka 50; Ujenzi wake umegharimu kiasi cha shilingi milioni
67.
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo(kwanza kulia) akipokea Kero kutoka
kwa mwananchi kama zilivyowasilishwa na Mama Debora wakati wa Unzinduzi
wa Daraja la Mto Kijenge.
Diwani
wa Kata ya jirani ya Themi, Melance Kinabo akizungumza kuhusu
changamoto zinazowakabili wakati wa uzinduzi wa Daraja la Mto Kijenge.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akizundua Daraja la Mto Kijenge.