|
AFISA
USTAWI WA JAMII WILAYANI TARIME MKOANI MARA SIWEMA SYLIVESTER AMBAYE PIA
NI MRATIBU WA KAMATI YA ULINZI WA MTOTO AKITOA MAFUNZO KWA WAJUMBE WA
KAMATI YA ULINZI WA MTOTO WEKIWEMO WENYEVITI WA VIJIJI KUTOKA KATA TA
MATONGO NYAMONGO. |
Ili kupinga
na kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa mtoto wa kike Wilayani Tarime
mkoani Mara zikiwemo Ndoa za Utotoni na ukeketaji ambao unatarajiwa kufanyika
mwaka huu Shirika la Plan
International kwa kushirikia na na Umoja wa nchi za ulaya, Jukwaa la utu wa
mtoto CDF, na Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF wamejengea uwezo
viongozi wa kamati ya ulinzi na haki za mtoto ngazi ya kata na vijiji wapatao 390 kwa lengo la kuendelea kutoa Elimu
juu ya kupinga mila na desturi zilizopitwa na wakati.
|
Viongozi hao
walipewa mafunzo hayo ni pamoja na Watendaji wa kata, Wenyeviti wa vijiji
kutoka kata za Sirari, Susuni, Sabasaba, Matongo na Nyamwaga kwa lengo la kuwa
mabalozi wazuri katika ngazi ya kata na vijiji ili kutoa Elimu ya kupinga
vitendo vya ukatili wa kijinsi ukiwemo Ukeketaji pamoja na ndoa za utotoni.
|
|
MRATIBU WA
MRADI WA KUPINGA NDO ZA UTOTONI , MIMBA ZA UTOTONI NA UKEKETAJI KUTOKA
SHIRIKA LA PLAN INTERNATINAL SHABAN SHABAN AKISAINI KITABU CHA WAGENI
KATIKA OFISI YA KATA YA MATONGO |
|
|
MAFUNZO YAKIENDEKEA |
|
AFISA USTAWI WA JAMII WILAYANI TARIME MKOANI MARA SIWEMA
SYLIVESTER AMBAYE PIA NI MRATIBU WA KAMATI YA ULINZI WA MTOTO AKISAINI KITABU CHA WAGENI BAADA YA KUFIKA KATAYA MATONGO |