BASATA WASEMA WAKOTIALI KUSULUHISHA BIFU YA DIAMOND NA KIBA LIKIFIKA MEZANI KWAO;
Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) limesema kwamba baraza hilo limesikia tetesi ya bifu ilioyopo kati ya wanamuziki nyota wawili nchini Alikiba na Diamond na kama wakipelekewa mezani kuhusu suala hilo watalishughulikia.
Katibu
Mkuu wa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA), Godfrey Mngereza amesema
amesikia kuna bifu kati ya Diamond na Alikiba lakini hawajapokea taarifa
rasmi ambayo inayoonyesha mmoja kati yao akilalamika kuhusu mwenzie.
Mngereza
amesema “Kwa upande wa serikali au BASATA tunafanya kazi kwa kuzingatia
maandishi au taarifa rasmi, kwahiyo suala (la Alikiba na Diamond)
halijatufikia rasmi,” alisema Mngereza. “Huu ni ushabiki au mashabiki
ndio wanaleta haya, kwa hiyo ni ushabiki wa team hii na hii na
tunaliona. Lakini kwa kuwa halijaja rasmi likija rasmi
tutalishughulikia,”
Pia
ameongeza kwa kusema kwamba “Lakini tukikutana na wao wenyewe wapo
safi, kwa hiyo wanaosababisha hivyo ni mashabiki kwa sababu hata
wachezaji wa Simba na Yanga wale ni wachezaji wapo kwenye tasnia moja,
ni marafiki wanakaa pamoja, wanakula pamoja ni kama wanamichezo wa
ngumi, wewe ukiwa nje unaangalia wao wanapigana kweli lakini ule ni
mchezo. Kwahiyo mimi hii naona ni ushabiki wa mashabiki ambapo kimsingi
huwezi kuwazua.
Diamond
na Alikiba ni wasanii nyota wanaofanya vizuri kwasasa ndani na nje ya
nchi lakini wamekuwa tofauti kutokana na mashabiki wao kugawanyika na
kufanya wasanii hao kuwa na tofauti na wasiopikika chungu kimoja.