YANGA YAIFANYA MBAYA KAGERA SUGAR YAIPIGA 6-2 KAITABA

 

Timu ya Yanga imeidhalilisha Kagera Sugar mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara kwa kuitandika jumla ya mabao 6-2 mechi iliyochezwa uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.

Ushindi huu ni watatu kwa Yanga ikiwa kanda ya ziwa na kuweza kuchukua alama 12 na kupoteza tatu kwani imezifunga Mwadui Fc 2-0,Toto African 2-0 na Kagera Sugar 6-2 na kupoteza mchezo mmoja bao 1-0 dhidi ya Stand United.

Kagera walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Mbaraka Yussuf dakika ya 3 hata hivyo halikudumu mnamo dakika ya 5 Donaldo Ngoma aliweza kuisawazishia alisawazisha baada ya kupokea pasi ya Msuva, Yanga waliliandama lango la wenyeji  dakika ya 21 Simon Msuva alifunga goli la pili na Obrey Chirwa la tatu dakika ya 25 hadi mapumziko Yanga walikuwa wako mbele kwa 3-1.

Kipindi cha pili kilianza kwa Kagera kufunga goli dakika ile ile ya tatu na mfungaji akiwa Yussuf huku likiwa la  pili kwa wenyeji, mnamo dakika ya 57 Deus Kaseke alifunga la nne kwa kazi nzuri ya Msuva.

Mshambuliaji aliyenunuliwa kwa pesa kubwa kuliko mchezaji yoyote wa Ligi Obrey Chirwa dakika ya 63 alifunga la tano kwa kazi nzuri ya Ngoma na kumfanya mchezaji huyo kufikisha magoli manne ya kufunga na dakika ya 72 Ngoma, aliiandikia la sita na kuwa mchezo wa kwanza kuwa na magoli mengi ya kufungana kuliko mechi zote za msimu huu.

Hadi mpira unamalizika Yanga wameibuka na ushindi wa jumla ya 6-2 na kufikisha pointi 21 kwenye msimamo wa Ligi kuu Vodacom wakati Mtibwa  wamebaki na pointi zao 18 na kuwa timu ya kwanza kufungwa magoli mengi kuliko timu yoyote msimu huu.

Yanga wanatarajia kurejea kesho Dar kwa ajili ya mchezo wao na Ruvu Shooting siku ya Jumatano uwanja wa Uhuru

Powered by Blogger.