Waziri Ummy atoa siku 60 wakurugenzi kuwapa wauguzi pesa za sare
Wakurugenzi
wa halmashauri na wale wa hospitali za umma nchini wamepewa siku sitini
kuanzia jana wawe wamewalipa posho za wauguzi za kununua sare za kazi
ya shilingi laki moja na elfu ishirini pamoja na malimbikizo ya sare
hizo.
Agizo
hilo limetolewa mkoani hapa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia
,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa 44
wa wauguzi Tanzania.
Waziri
Ummy alisema asilimia themanini ya kazi zote kwenye sekta ya afya
nchini zinafanywa na wauguzi,hivyo aliwataka wakurugenzi kuzingatia
miongozo iliyopo ya Serikali, “kama mwongozo ni kulipa elfu thelatini
lipa thelathini si vinginevyo. Serikali imekwishatoa waraka wa kazi za
ziada yaani “extra duty circular” ambao unapaswa kufuatwa hata
mnapofanya kazi usiku kwani kuna masaa ya ziada”.
“Nawaagiza
waajiri wote kuzingatia nyaraka hizi ili kuondoa malalamiko yasiyo ya
lazima, Hili ni suala muhimu kwani mnakuwa kazini siku tano hadi sita
kwa wiki hivyo mnahitaji sare walau tano ili muweze kubadilisha kila
mara. Serikali itatoa waraka wa si chini ya laki tatu kulingana na hali
ya uchumi itavyokuwa. Natumaini waraka huu utatoka mapema na kuanza
kutumika mwaka ujao wa fedha hivyo kwa mwaka huu tuendelee kutumia
waraka uliopo.
Aidha,
aliagiza baada ya siku sitini alizotoa kupatiwa orodha za halmashauri
ambazo hazitokuwa zimewalipa posho hizo na mikoa ipi”kwani kuna wauguzi
wangapi hadi mshindwe kuwapa posho za sare ,mnataka wauguzi hawa waje
kazini wawe wamevaa nini?aliuliza Waziri
Akijibu
tatizo la kusimamishwa na kufukuzwa kazi kwa wauguzi na wakunga alisema
,suala la kusimamisha au kumwachisha kazi mtumishi lina taratibu zake
ambazo zinapaswa kufuatwa.
“Napenda
kuliagiza Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania kuwaelimisha waajiri
kuhusu hatua za kufuata katika kushughulikia malalamiko yanayotolewa na
wananchi ili yaweze kusikilizwa kwa utaratibu zilizopo bila ya kuwaonea
pande zote, Ni kweli kuwa unapoadhibiwa bila kosa inavunja moyo, Naomba
ieleweke kuwa sio nia ya Serikali kuwaumiza wauguzi bali lengo letu
kubwa ni kuondoa kero za wananchi ikiwa ni pamoja na kuwashughulikia
watumishi wote wazembe na wasiofuata maadili ya kazi”.
Hatahivyo
Waziri huyo ametoa rai kwa jamii kuweza kuwaheshimu wauguzi na wakunga
kwani kumtukana na kumnyanyasa ni kutomtendea haki kwani wauguzi
wanatakiwa kupendwa na kuthaminiwa”wahenga walisema usitukane mkunga na
uzazi ungalipo,hivyo wananchi msiwatukane wauguzi kwani mkeo au mtoto
wako atajifungua na atasaidiwa na huyo mkunga,tuwapende na kuwaheshimu
wauguzi”.
Aliwataka
Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuweka namba maalumu za wananchi kutoa
malalamiko na kwa upande wa viongozi kuondoa urasimu wa kushughulikia
malalamiko hayo kwa kuweka utaratibu mzuri wa kuwashughulikia ambayo
yamezidi na yanakatisha tamaa kwa kada hiyo.
Kuhusu
upungufu mkubwa wa wauguzi Waziri Ummy alisema ni kweli kuwa, nchi
inakabiliwa na changamoto kubwa ya uhaba wa wauguzi hali inayopelekea
muuguzi mmoja kuhudumia wagonjwa wengi zaidi ya uwezo wake,Mazingira
hayo yanaweza kuathiri ubora wa huduma wanayotoa.
“Serikali
inaendelea na jitihada za kuhakikisha watumishi wa afya wenye weledi wa
kutosha wakiwamo wauguzi wanapatikana na kupangiwa katika vituo vya
kazi sehemu mbalimbali za nchi yetu, Napenda nitumie fursa hii
kuwahakikishia kuwa Serikali imepanga kuongeza idadi ya wauguzi nchini
kila mwaka mara tu zoezi la kuwaondoa watumishi hewa kukamilika
ninaamini Sekta ya Afya itapewa kipaumbele cha kwanza katika ajira mpya.
Hivyo, niwaombe muendelee kuwa wavumilivu na kutoa huduma vema kwa
kuzingatia taaluma yenu wakati jitihada za kuongeza watumishi
zikiendelea”.
Wauguzi
nchini wamekuwa na utaratibu wa kukutana kitaifa na kuelimishana juu ya
maadili,majukumu ya viongozi wa chama katika utoaji wa huduma za afya
kwa weledi kwa magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza.Mkutano
umebeba ujumbe maalumu na kauli mbiu ya mwaka huu ni “Wauguzi :nguvu ya
mabadiliko,uboreshaji wa uthabiti wa mfumo wa afya.