Wakazi wa kijiji cha Kipamba, Singida waandikishwa kupata mgao wa TASAF
Jumla
ya Wahadzabe 136 kati ya 138 wakazi wa kijiji cha Kipamba wilaya ya
Mkalama mkoani Singida,wameandikishwa kwenye mpango wa kunusuru kaya
maskini TASAF 111 na wamenza kufaidika kuanzia Septemba mwaka huu,hadi
sasa.
Kundi
la kabila la Wahadzabe ambalo linadaiwa kuwa limesahaulika,bado
linaishi maisha ya kijima na linategemea asali,matunda pori,mizizi ya
miti na nyamapori kama ndio chakula chao kikuu.
Imedaiwa
kuwa kutokana na changamoto za tabia nchi na makundi ya wafugaji
kuvamia pori la kijiji cha Kipamba,vyakula hivyo vya asili,havipatikani
kwa kiwango cha kukidhi mahitaji.
Hayo
yamesemwa mwishoni mwa wiki na mratibu wa TASAF mkoa wa Singida,Patrick
Kasango,wakati akitoa taarifa yake ya utekelezaji wa mpango wa TASAF
111, mbele ya wawakilishi kutoka benki ya dunia,shirika la kazi dunia
(ILO) na UNDP ambao wamefanya ziara ya kikazi mkoani hapa, kukagua
utekelezaji wa TASAF.
“Lengo
kuu la kuandikisha kundi la Wahadzabe katika mpango huu wa TASAF 111,ni
kulisaidia kundi hilo kuanzisha miradi ya ufugaji kuku na mbuzi,ili
kujipatia kipato.Pia kuongeza mahudhurio shuleni kwa watoto wa kundi
hilo, pamoja na vituo vya kutolea huduma za afya.Vile vile kuongeza
mahudhurio ya akina mama kuhudhuria kliniki”,alifafanua Kasango.
Katika
hatua nyingine,Mratibu huyo,alisema kuwa TASAF 111 mkoani hapa,imetumia
zaidi ya shilingi 18.8 bilioni kwa ajili ya kunusuru kaya masikini
40,218, kati ya septemba mwaka huu,hadi sasa.
Hata hivyo,alisema kuwa kaya 281 zimeondolewa katika mpango huo kutokana na sababu mbalimbali,ikiwemo ya vifo vya walengwa.
Kati
ya fedha hizo,shilingi 430,357,208.08,zimetumika kugharamia ujenzi wa
zahanati nne na nyumba mbili za kuishi watumishi wa afya na elimu.
Aidha,alisema
fedha zingine shilingi 562,755,000 zimetumika kununulia vifaa
vinavyotumika kwenye miradi ya ujenzi inayotoa fursa za ajira za muda
kwa walengwa.
“Ajira
hizi za muda,zimelenga kuziongezea kipato kaya zilizoandikishwa kwenye
mpango wa TASAF 111 na wakati huo huo,kaya hizo zitakuwa zimeshiriki
kuondoa kero zinazowakabili katika maeneo yao,ikiwemo uhaba mkubwa wa
maji”,alisema.
Mratibu
Kasango alisema pamoja na mafanikio hayo ya kujivunia,bado wanakabiliwa
na changamoto mbali mbali,ikiwemo ya uhaba wa magari, barabara mbovu
ambazo wakati wa masika,hazipitiki na baadhi ya kaya kutembea mwendo
mrefu kufika kwenye kituo cha kuhaulisha fedha na baadhi ya maeneo
kutokuwa na huduma za simu.
Mwenyekiti
wa kijiji cha Kipamba Edward Mashimba Mkumbo,pamoja na kuipongeza
serikali na wadau wengine,kwa kulishirikisha kundi la Wahadzabe kwenye
mpango wa TASAF 111, ameiomba serikali kuwajengea barabara ya kupitika
wakati wote.
“Kama
mpango huu usingeanzishwa huku kwetu,hali ingekuwa mbaya sana kwa
sababu vyakula vyetu vya asili,havipatikani tena. Na sisi kama
mnavyojua, hatuna utamaduni wa kulima. Niiombe tena serikali itupatie
wahudumu wa afya akidai kwamba toka jengo la zahanati yao likamilike
miaka kadhaa iliyopita,hawajapatiwa mhudumu.Pia tupatiwe hati miliki ya
eneo letu,” alisema.
Kwa
upande wake mkurugenzi uratibu TASAF makao makuu, Alphonce
Kyariga,ameishauri TASAF mkoani hapa, kuhakikisha taarifa zao zinakuwa
na takwimu, kwa madai kwamba zikiwa na takwimu, zitakuwa chachu kwa
serikali na wadau wengine kuzipatia ufumbuzi wa kudumu changamoto
husika.
Naye
mwakilishi wa benki ya dunia,Wolter Soer,alisema kwa kiwango
kikubwa,timu yao imeridhishwa na utekelezaji wa TASAF mkoani Singida,na
kuahidi kwamba wataendelea kushirikiana na serikali ya awamu ya tano,
kuendeleza mpango huo.
“Kwa
upande wa kundi la Wahadzabe,tumeguswa zaidi na kwamba tutachukua hatua
maalum katika kulisaidia kundi hili.Tunataka ifike wakati na Wahadzabe
wawe na maisha bora kama walivyo Watanzania wengine,” alisema Soer.