SHINDANO LA MISS TANZANIA 2016 JIJINI MWANZA KUWA BORA ZAIDI.
Leo Oktoba 19,
2016 Kamati ya Shindano la Maandalizi ya Miss Tanzania 2016 imesema
Shindano hilo linalotarajiwa kufanyika Oktoba 29,10, 2016 katika viunga
vya Rock City Jijini Mwanza, litakuwa bora zaidi kutokana na maandalizi
yaliyofanyika na yanayoendelea kufanyika.
Mwenyekiti wa
kamati hiyo, Hashim Lundenga (kulia) ambaye pia ni Mkurugenzi wa kampuni
ya Rhino Agency inayoandaa Miss Tanzania, amesema baada ya mashindano
hayo kufanyika Jijini Dar es salaam miaka yote, kamati hiyo imeamua
yafanyike Jijini Mwanza na kwamba yatafanyika kwa miaka mitano
mfululizo.
Amesema
washiriki wote 30 katika shindano hilo ni bora hivyo yeyote atakayeibuka
mshindi ataliwakilisha vyema taifa kwenye mashindano ya Miss World
yanayotarajiwa kufanyika Disemba 18, 2016 Jijini Washingtone DC nchini
Marekani.
Viingilio
katika shindano hilo ni shilingi 20,000, 50,000 na 100,000 ambapo
inategemewa kwamba wasanii Ali Kiba pamoja na Christian Bella ikiwa
wataafiki makubaliano watadondosha burudani katika shindano hilo huku
washiriki wakijipatia fursa mbalimbali ikiwemo mshindi wa kwanza
kujishindia gari.
Washiriki wa
shindano hilo wamesema wamejiandaa vyema na bado wanaendelea kujinoa
zaidi ili kuhakikisha atakayeibuka mshindi anaiwakilisha vyema Tanzania
kwenye mashindano ya dunia huku wakielezea furaha yao kubwa kwa
mashindano hayo kufanyika Jijini Mwanza kwa mara ya kwanza.
Kamati ya Miss Tanzania 2016 ambapo kutoka kulia ni Hashim Lundenga, Pamela Irengo, Flora Lauwo.
Mkutano baina ya Kamati ya Miss Tanzania 2016 na Wanahabari Jijini Mwanza
Washiriki wa Miss Tanzania 2016 katika ubora wao
PICHA NA BMG