SERIKARI YATAKIWA KURUDISHA MUDA WA ZAMANI WA KUFUNGUA BAA.
Mwenyekiti wa Chama cha Wahudumu wa Baa
Tanzania (Chawabata), Ali Hussein (kulia), akizungumza jana na
waandishi wa habari Dar es Salaam, wakati akitoa ombi kwa serikali la
kuomba kufunguliwa baa muda wote ili kunusuru biashara hiyo. Kushoto ni
Katibu wa chama hicho, Boniface Lameck.
Katibu wa chama hicho, Boniface Lameck. akisisitiza jambo kwenye mkutano huo.
CHAMA
cha Wahudumu wa Baa Tanzania (Chawabata) kimeiangukia serikali kwa
kuiomba iruhusu wenye mabaa kufanya biashara zao wakati wote ili
kusaidia kupata fedha za kulipa kodi na mishahara ya wafanyakazi wao.
Ombi
hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Ali Huseein
wakati akizungumza Jijini Dar es Salaam jana kuhusu changamoto waliyonao
wenye mabaa katika kufanya biashara yao hiyo ya uuzaji wa vileo na
vinywaji baridi.
"Tunaiomba
serikali kuangalia kwa karibu kuhusu muda wa kufungua baa kwani muda
huu wa sasa wa kufungua saa 10 jioni na kufunga saa tano ni mdogo
ukilinganisha na ilipokuwa awali wa kufungua wakati wote" alisema
Hussein.
Hussein
alisema nia ya serikali haikuwa mbaya ya kufungua baa saa 10 lakini
hawakuangalia upande wa pili wa wamiliki wa baa hizo kwani wengi wao
kwani katika muda huo wengi wao hawafanyi kabisa biashara.
Aliongeza
kuwa wafanyabiashara hao wanahitaji kupata muda wa siku nzima wa
kufanya biashara zao ili waweze kumudu kupata fedha za fedha za kulipa
kodi ya serikali na mishahara ya wafanyakazi na wahudumu wa baa ambao ni
wengi ambapo hivi sasa wanashindwa kufikia malengo.
Alisema
baadhi ya baa zimepunguza wahudumu wake kutokana na kubanwa na muda huo
ambapo wahudumu wamekuwa wakiingia jioni tu baada ya muda wa asubuhi
kupigwa marufuku na serikali.
"Wenye
mabaa hivi sasa wapo katika changamoto kubwa ya biashara zao tunaiomba
serikali kuangalia jambo hilo kwa sura nyingine ili kuinusuru biashara
hiyo kuanzia mmiliki wa baa na viwanda vinavyotengeneza bidhaa hiyo na
serikali yenyewe kupata kodi yake.
Alisema
kuwa changamoto hiyo waliibaini baada ya kuzitembea baa kadhaa jijini
Dar es Salaam mapema mwezi huu ambapo walipata fursa ya kuzungumza na
wamiliki wa baa na wahudumu wa baa hizo.
Katibu
wa chama hicho, Boniface Lameck alisema kutokana na kubanwa kwa muda wa
kufungua baa kumepunguza ajira kwa wahudumu wa baa nyingi hapa nchini
ambao ni wadau wao wakubwa wa viwanda vya bia na wamiliki wa baa.
Alisema bila ya wahudumu wa baa biashara hiyo inakuwa inapoteza kundi muhimu la kuzifanya bia hizo kusambaa katika soko.
"Tunaiomba
serikali kuruhusu baa kufunguliwa wakati wote kama ilivyokuwa zamani
jambo litakalosaidia wenye mabaa kupata fedha za kulipa mishahara na
kodi " alisema Lameck.
Lameck
aliongeza kuwa muda uliotengwa na serikali ni kama masaa saba tu
kuanzia saa 10 hadi saa tano usiku na ndani ya muda huo wateja wengine
wanaondoka kuanzia saa moja hadi saa tatu hivyo kuwa changamoto ya
biashara hiyo.