Serikali imesema itaendelea kuimarisha ushirikiano na maelewano mazuri yaliyodumi kwa miaka 50 kati ya Tanzania na Uswizi
Serikali imesema itaendelea kuimarisha ushirikiano na maelewano mazuri yaliyodumi kwa miaka 50 kati ya Tanzania na Uswizi hususani katika nyaja ya maendeleo ikiwemo kujenga uchumi kati ya nchi hizo mbili.
Akizungumza wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya ushirikiano wa kidplomasia kati ya Uswizi na Tanzania vilivyoambata na uzinduzi wa kitabu cha maonyesho ya kazi za wasanii waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki ,kikanda na kimataifa Dk. Augustine Mahiga amesema katika kipindi cha miaka 50 iliyopita Tanzania na Uswizi zimejega ushirikiano mzuri kupitia majadiliano ya kisiasa ,kiuchumi na maendeleo katika shughuli za kiutamaduni.
Dk. Mahiga amesema Uswizi imeendelea kufanya kazi na washirika wa Tanzania ili kusaidia kuleta usawa wa kijamii ,ukuaji wa uchumi na kupunguza umasikini katika mikoa ya hapa nchini kupitia sekta tatu za afya ,ajira na kipato na utawala.
Kwa upande wake balozi wa Uswizi nchini bi.Florence Mattli amesema kupitia juhudi za ushirikiano kati ya Tanzania na Uswizi umeleta mafanikio mengi ikiwemo maendeleo katika sekta ya afya .