Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Tandahimba amempa siku 10 mfugaji Sadick Athuman

drought1
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Tandahimba ambae pia ni mkuu wa wilaya hiyo Sebastian Waryuba amempa siku kumi mfugaji Sadick Athuman mwenye kundi la ngíombe zaidi ya mia nne na hamsini kuhama wilayani humo baada ya kuanza kuleta migogoro baina yake na wakulima wa kijiji cha Lipalo B.

Mfugaji huyo ambaye ameingia ndani ya wilaya ya Tandahimba bila kufuata taratibu za kisheria tayari ndani ya siku sita alizokaa amelisha mifugo yake mazao ya wakulima zaidi ya kumi na tatu na kusababisha migogoro.
Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Tandahimba inawasili katika kijiji cha Lipalo B ambapo bwana Sadick Athuman ameweka kambi ya zaidi ya ngíombe mia nne na hamsini,
Kamati hiyo imefika kufuatia wakulima kulalamika mazao yao kuharibiwa na kundi la ngíombe hao.
Kufuatia malalamiko hayo ambayo si kawaida kutokea kwa wakazi wa wilaya ya tandahimba kutokana na kujihusisha moja kwa moja katika kilimo hasa cha mikorosho,mkuu wa wilaya hiyo Sebastian Waryuba anamtaka Sadick kuhama ndani ya siku kumi baada ya kulipa fidia kwa wakulima walioharibiwa mazao yao.
Kwa upande wake mfugaji wa ngíombe hizo Sadick Athuman amekiri kuingia wilayani humo bila kibari akitokea wilaya ya Nanyumbu,na kwamba kundi la ngíombe zaidi ya mia nne hamsini ni kati ya makundi matatu aliyoyaweka sehemu mbalimbali.
Powered by Blogger.