Msamaha wa Mwalimu wa ‘field’ Frank Msigwa wazua maswali mitandaoni


Baada ya kufukuzwa Chuo kwa hatua yao ya kushiriki kitendo cha kumpiga mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya kutwa ya sekondari mkoani Mbeya (Mbeya Day), Mwanafunzi Sebastian Chingulu tamko lililotolewa na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof. Joyce Ndalichako , Mwalimu Frank Msigwa  hatimaye ameibuka na kuomba msamaha kwa Watanzania.
Frank Msigwa kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram, (frank_msigwa_) ambayo hadi leo Oktoba 10.2016 akaunti hiyo imeweza kupata Followers 741 na Following  ikifikia 2065,   huku akiwa ameposti mara m ili tu ikiwemo post yake ya jana Oktoba 9 juu ya tamko lake hilo la kuomba msamaha na leo kupost tamko la kusikitishwa kwake kwa Watanzania walivyopokea msamaha wake huo. (Angalia picha).
Hata hivyo, mtandao huu wa MUSSA MAKALI BLOG, imeweza kufuatilia maoni mbalimbali ya watanzania kupitia mitandaoni ikiwemo ile ya WhatsApp, Facebook, Instagram na mingineo, watu mbalimbali wamekuwa wakichukulia tofauti msamaha wake huo na hata wengine wakiubeza kuwa ni akaunti ‘feki’ ya Mwalimu huyo Mwanafunzi Frank  Msigwa.
Mbali na kuona suala hilo la msamaha kwa kijana huyo kupitia mitandao ya kijamii watu mbalimbali wameeleza kuwa alipaswa kwenda kwenye vituo vya radio na TV kuomba msamaha huo huku wengine wakimtaka aende kwa wazazi wa mtoto aliyepigwa ndio wataweza kumsamehe.
Kwa hali hiyo hadi sasa bado Frank Msigwa anazua maswali mengi kwa wananchi kama ni kauli yakke kutoka kinywa chake ama ni mtu ameamua kufanya hivyo kwa niaba ya Msigwa?..
Tutakuletea hapa zaidi, endapo tutawasiliana na Frank Msigwa kututhibitishia hilo.
Powered by Blogger.