LHRC YAFUNGUA KESI DHIDI YA SERIKALI KUPINGA ADHABU YA KIFO
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk.Helen Kijo- Bisimba (katikati), Mkurugenzi wa Uwezeshaji na Uwajibikaji, Imelda Urio (kulia) na Mkurugenzi wa Utetezi na Maboresho wa LHRC, Anna Henga , wakionesha jarida la kupinga adhabu ya kifo wakati wa uzindi wake Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk.Helen Kijo-
Bisimba (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari
Dar es Salaam leo, wakati akisoma tamko la kupinga adhabu ya kifo. Kulia
ni Mkurugenzi wa Uwezeshaji na Uwajibikaji, Imelda Urio na kushoto ni Mkurugenzi wa Utetezi na Maboresho wa LHRC, Anna Henga.
Mkurugenzi wa Uwezeshaji na Uwajibikaji, Imelda Urio (kulia), akisisitiza jambo kwenye mkutano huo.
Mkurugenzi wa Utetezi na Maboresho wa LHRC, Anna Henga akizungumza katika mkutano huo.
Mkutano na waandishi wa habari ukiendelea.
Mkutano na waandishi wa habari ukiendelea.
………………………………………………………..
Na Dotto Mwaibale
KITUO
cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimefungua kesi ya kikatiba
kuhusiana na ulinzi wa haki ya kuishi na urekebishwaji wa sheria ya
kanuni ya adhabu juu ya ulazima wa kutolewa kwa adhabu ya kifo katika
makosa ya uhaini na mauaji.
Kesi
hiyo imefunguliwa dhidi ya mwanasheria mkuu wa serikali wakitaka
ufafanuzi zaidi juu ya adhabu ya kifo, wakibainisha kuwa adhabu hiyo
haimpi nafasi mtuhumiwa kujirekebisha bali ni ya kulipiza kisasi.
Kituo
hicho kimesema endapo Tanzania itatekeleza hukumu ya kifo kwa sasa
inamaanisha watu wapatao 228 na zaidi watapoteza maisha yao huku
wengine 244 wanasubiria maamuzi ya rufaa zao.
Akizungumza
wakati akitoa tamko la kupinga adhabu ya kifo Dar es Salaam leo
Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Hellen- Kijo Bisimba alisema hadi mwaka
2015 jumla ya watu 472 walikuwa wamehukumiwa kunyongwa.
Alisema
kituo kinaiomba serikali kurekebisha sheria ya kanuni ya adhabu na
sheria ya ugaidi yenye kutoa adhabu ya kifo kwa makosa ya mauaji, uhaini
na ugaidi.
Dk.
Bisimba alisema kituo kina sababu za kupinga adhabu hiyo ya kifo na
hawafurahii watu kuua wengine na ndio maana hawapendi pia hata muuaji
auawe.
“Adhabu
ya kifo ni vigumu kuhakikisha kuwainatekelezwa tu kwa wale watu ambao
huwezi kuirekebisha kwani mfumo wa utoaji haki huwa pia na mianya ya
makosa na hivyo maisha ya mtu yanaweza kupotea bure,” alisema Dk.
Bisimba na kuongeza kuwa hakuna ushahidi wowote kuwa adhabu hiyo inaweza
kuzuia watu wengine kutokutenda makosa kama hayo.
Alisema
licha ya adhabu hiyo kutokutekelezwa nchini kwa takriban miaka 22 ,
taaarifa zinaonesha kuwa watu 72 ambao walishawahi kunyongwa kutokana na
adhabu hiyo.
Hata
hivyo aliiomba serikali kutengeneza utaratibu wa kuelimisha jamii juu
ya kuheshimu haki za binadamu hususani haki zakuishi na kuweka mazingira
ya kuiheshimu haki hiyo, pia ibadilishe sheria kwa kuondoa adhabu ya
kifo na kuweka adhabu mbadala kwenye makosa ya jinai na kwa wafungwa
waliopo mfano vya muda mrefu gerezani.