Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la "Lumala
Mpya International Church" lililopo Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza,
Dkt.Daniel Moses Kulola, anawahimiza watu wote kufika kwenye tamasha la
Kusifu na Kuabudu linalofanyika hii leo kanisani hapo.
Dkt.Kulola amesema watu wote watakaofika
kwenye tamasha hilo ambalo litaanza majira ya saa nane mchana leo
Oktoba 09,2016, watabarikiwa na kufunguliwa kiroho na hivyo kuwa huru na
vifungu vinavyowatesa.
|