Kichuya mchezaji Bora VPL kwa mwezi Septemba
Mshambuliaji
Shiza Kichuya (pichani) wa Simba SC amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa
Ligi Kuu ya Vodacom kwa Septemba msimu wa 2016/2017.
Kichuya ambaye ni mshambulaji aliwashinda wachezaji Adam Kingwande wa Stand United na Omari Mponda wa Ndanda FC.
Mchezaji
aliisadia timu yake kwa mwezi huo kupata pointi zote 12 katika mechi
nne ilizocheza, matokeo ambayo yameifanya Simba iendelee kuongoza Ligi
hiyo inayoshirikisha timu 16. Pia alifunga mabao matatu katika mechi
mbili kati ya nne ilizocheza timu yake.
Kwa
kushinda tuzo hizo ya mwezi, Kichuya atazawadiwa kitita cha sh.
1,000,000 (milioni moja) kutoka kwa wadhamini wa Ligi hiyo, kampuni ya
Vodacom Tanzania.