HALMASHAURI YATENGA MILLIONI 450 KUBORESHA MIUNDOMBINU YA ELIMU MSINGI
MWENYEKITI WA HALMSHAURI YA WILAYA YA TARIME MISIWA YOMAM AKIONGEA NA VYOMBO VYA HABARI HII LEO OFISINI KWAKE |
KULIA NI AFISA ELIMU MSINGI HALMASHAURI YA WILAYA YA TARIME EMMANUEL JONHNSON AKITEATA JAMBO NA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA TARIME MISIWA |
WAANDISHI WA HABARI WAKIWA KAZINI |
Halmashuari ya wilaya ya Tarime Mkoani Mara imetenga
Millioni 450 kwa ajili ya kuboresha na kukarabati Miundo mbinu ya Elimu katika
shule za msingi ili kuwepo kwa mazingira mazuri ya Ufundishaji na ufundishwaji
jambo ambalo litakuwa ni chachu ya kuongeza ufaulu kwa Wanafunzi.
Akiongea na waandishi wa habari hii leo ofisini kwake
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Moses Misiwa Yomam amesema kuwa
fedha hizo zimetengwa kwa ajili ya kuborsha miundombinu ya Elimu hususani vymba
vya madarasa ambavyo vimejengwa kwa nguvu za wanachi.
Misiwa amesema kuwa Halmashauri yake imeweza kumamaliza
changamoto ya upungufu wa madawati katika shule za msingi ambaopo Halmashauri hiyo
imetekeleza zoezi la madawati kwa asilimia miamoja bila kuchangisha mwananchi
bali wachangiaji ni wadau wa Elimu ukiwemo Mgodi wa Uchimbaji wa dhahabu
Nyamongo Acacia
Aidha Mwenykiti amesema kuwa fedha hizo zimelenga kumalizia
maboma ya madarasa katika shue sitini na nyingine kumalizika badae.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashuari ya wilaya ya
Tarime Emmanuel Jonsonambaye ni ASfisa Elimu Msingi kwa niaba ya mkurugenzi wa
Halmashauri hiyo Apoo Castro Tindwa amesema kuwa Halmashauri inathamini
ushiriki wa wananchi katika suala la maendeleo na fedha hizo zimetengwa kwa
ajili ya kukamilisjha maboma ya madarasa ili yaweza kufanya kazi mara moja.
Emmanuel ametoa witoa kwa wananchi kuwa suala hilo liwe
chachu ya kuendelea kuborsha miundombinu ya Elimu kwa lengo la kutatua
chngamoto ya upungufu wa madarasa katika shule za Msingi na kuongeza ufaulu kwa
wanafunzi
Hata hivyo Afisa Elimu Msingi amezungumzia suala zima la Changamoto
ya upungufu wa Nyumba za walimu, pamoja na matundu ya Vyoo katika shule za
Msingi ambapo amesema kuwa kwa sasa Halmashauri imeanza na suala la madawati na
sasa wanaingia kukarabati maboma na badae wataangalia suala la Nyumba za Walimu
na Vyoo kwa ujumla.
ZABRON MRIMI KATIBU WA MBUNGE JIMBO LA TARIME VIJIJINI JONH HECHE |