DAKTARI WA ZAMU ALALAMIKIWA NA WAGONJWA WILYANI MUSOMA
BAADHI ya wagonjwa wanaofika kutibiwa katika hospitali ya
rufaa ya mkoa wa Mara mjini Musoma wamelalamikia kitendo kilichofanywa na
daktari wa zamu kushindwa kuwapa matibabu kwa wakati kutokana na kile
alichowaeleza nyakati za jioni hospitali hiyo hupokea na kutibu wagonjwa wa
dharula.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hii walisema kuwa tukio hilo
linadaiwa kutokea jana saa 10 jioni ambapo wagonjwa hao walifika hospitalini
hapo kwa ajili ya kupata matibabu, lakini walishangazwa baada ya kufika chumba
cha mapokezi na kupokelewa kwa kutozwa sh. 10000 ya kumwona daktari.
Mariamu Mafuru ni miongoni mwa wagonjwa hao alisema alifika
hapo akiwa anasumbuliwa na maumivu makali ya tumbo kutokana na ukubwa wa
hospitali hiyo alitegemea kupata matibabu mazuri kufuatia kulipa fedha hiyo
aliyoeleza ni ya kuonana na daktari lakini alikaa takribani masaa mawili bila
kuonana na daktari huyo .
‘’Yaani tumekaa sana baada ya kutoka mapokezi tuliambiwa
tuje chumba namba moja ambapo ndipo daktari yupo baada ya kufika hapa daktar
alikuwa na mazungumzo na mgonjwa mwingne lakini baada ya kumalizana na huyo
mgonjwa alitoka nje nakutuambia huu muda wapokei wagonjwa kama sisi eti
wanatibu wagonjwa wadharula’alisema na kuongeza kuwa ………………
‘’kitendo alilichokifanya ni kibaya kwa kweli anatuambia
yule mgonjwa aliyeumwa na nyoka ndio wa kumuhudumia na wagonwa wa kipindupindu,
wanaoharisha,walioletwa na ambulace lakini sio sisi hatujafurahishwa na majibu
yake’’alisema huku akilia Mariamu.
Kwa upande wa daktari huyo aliyejitambulisha kwa majina ya
Paul Masse alisema kulingana na mida na masaa waliokuja wagonjwa hao
hawastahili kupokelewa hata kupewa huduma kwakuwa wamekuja kwa kujisikia muda
huo huwa anabaki daktari mmoja ambaye ana shughulikia emergence case wagonjwa
wa dharula.
‘’Haiwezekani kabisa kuwa hudumia wagonjwa hawa yaani mtu
anakuja kupata matibabu muda huu..? ofisi zote zimeshafungwa ukizingatia mimi
ndo daktari niliyebaki wa zamu ndo maana kuna hospitali nyingine huko hawa
inabidi waanzie Nyasho,Bweri hata kigera ndizo waende huko sasa hivi mimi na
hudumia wagonjwa wa dharula kama kipindupindu,huyo aliyegongwa na nyoka na
wanaojifungua sio hawa alisema daktari huyo’’.
Licha ya kutolewa kauli hiyo waliodai kutofurahishwa nayo
wagonjwa waliendelea kukaa kwa muda wa masaa mawili bila kuondoka mpaka daktari
huyo aliporejea katika chumba kile na kuanza kuwatibu huku kwa kuwafokea
kutokuja kupata matibabu muda huo nakwamba wafike mida ya asubuhi saa mbili
hadi saa nane.