MOTO WATEKETEZA MSITU UFYOMI MLIMA WA KWARAA BABATI**

 



Msitu wa Ufyomi uliopo katika Mlima wa Kwaraa, wilayani Babati mkoani Manyara, unateketea kwa moto ulioanza Oktoba 25, 2026. Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wamefika katika eneo hilo kwa ajili ya kukabiliana na moto huo.


Chanzo cha moto huo kinadaiwa kuwa ni shughuli za kibinadamu, ambapo baadhi ya wananchi wanaoishi karibu na msitu huo wanahusishwa na uchomaji wa moto kwa lengo la kuchochea uotaji wa majani mapya kwa ajili ya malisho ya mifugo wakati mvua zinapoanza kunyesha.


Kwa mujibu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, asubuhi ya leo, Oktoba 26, 2026, limeongeza nguvu katika juhudi za kuudhibiti moto huo ili kuzuia usisambae na kuathiri makazi ya wananchi wanaoishi karibu na eneo hilo.


Hadi sasa, hakuna athari zilizoripotiwa katika makazi ya watu, ingawa moto huo umesababisha uharibifu wa mazingira. Wakati huo huo, TFS inaendelea kufanya tathmini ili kubaini ukubwa wa eneo lililoteketea kwa moto huo.

Powered by Blogger.