WANANCHI JAMII YA WAFUGAJI KUNUFAIKA NA MAJI SAFI

 


Zaidi ya wananchi 3,000 pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Ormotoo na wafugaji katika Kitongoji cha Ormotoo, Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara, wanatarajiwa kunufaika na mradi wa kisima cha maji uliotekelezwa na Shirika la EKRAT.

Mradi huo umekabidhiwa kwa Serikali na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Manyara ambaye pia ni Mwenyekiti wa Shirika la EKRAT, Peter Toima, huku ukitarajiwa kupunguza changamoto ya wananchi kusafiri umbali wa zaidi ya kilomita tano kufuata maji.





Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Toima amesema Shirika la EKRAT limeendelea kushirikiana na Serikali katika kutekeleza miradi ya maendeleo, ikiwemo ujenzi wa shule na miradi ya maji, kwa lengo la kuboresha maisha ya wananchi.


Aidha katika hatua nyingine amesema shirika hilo tayari limejenga na kukabidhi kwa Serikali zaidi ya shule 70 katika maeneo mbalimbali nchini.

Powered by Blogger.