RPC TARIME/RORYA AWATAKA ASKARI KUIMARISHA USHIRIKIANO NA JAMII
Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi Tarime Rorya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Mark Njera, amewataka Askari kuimarisha ushirikiano na jamii katika kubaini, kuzuia na kutanzua uhalifu.
Kamanda Njera ametoa rai hiyo wakati akizungumza na askari katika Baraza la Askari baada ya ukaguzi katika Wilaya ya Polisi Nyamwaga, ambapo amesisitiza umuhimu wa askari kuwa karibu na wananchi ili kujenga uaminifu na kuwawezesha kutoa taarifa za uhalifu kwa wakati.
Aidha, amewataka Askari kutekeleza majukumu yao kwa weledi, nidhamu na uadilifu, pamoja na kutoa elimu kwa jamii kuhusu masuala ya ulinzi na usalama.
