MSIBA MZITO MUSOMA VIJIJINI
TANZIA TANZIA TANZIA
Kijiji cha Nyasaungu kimeondokewa na Mdau Mkuu wa
Maendeleo yao
Kwa masikitiko na majonzi mengi mno ninalazimika kutoa
taarifa ya kifo cha mpendwa wetu Ndugu STEPHEN CHACHA MWITA WAMBURA (picha
imeambatanishwa hapa)
Marehemu alipatwa na mauti kwenye ajali ya gari
iliyotokea usiku wa Alhamisi (28 Nov) kuamikia Ijumaa (29 Nov) Jijini Mwanza!
Marehemu Chacha Mwita alikuwa Kiongozi wa jamii,
Mchangiaji mkuu wa miradi ya maendeleo na Kada wa CCM.
Marehemu alichangia miradi yote muhimu ya Kijiji cha
Nyasaungu:
1. Marehemu alikuwa mchangiaji mwanzilishi wa ujenzi
wa S/M Nyasaungu
2. Marehemu alishirikiana na Mbunge wa Jimbo kwenye
michango ya uboreshaji wa S/M Nyasaungu
3. Marehemu alikuwa mchangiaji mwanzilishi wa ujenzi
wa Zahanati ya Kijiji cha Nyasaungu
4. Marehemu alishirikiana na Mbunge wa Jimbo
kuendeleza ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Nyasaungu
Tunaishukuru Serikali yetu kwa kuchangia Tsh milioni 100 (Tsh 100m)
kukamilisha ujenzi wa Zahanati hiyo itakayofunguliwa Januari 2025
5. Marehemu alishirikiana na Mbunge wa Jimbo kuanza
kuchangia ujenzi wa Nyasaungu Sekondari ambayo imepangwa kufunguliwa Januari
2025
Poleni Wana-Nyasaungu tumempoteza mwenzetu
tuliyeshirikiana nae kwa ukaribu sana kuchangia maendeleo na ustawi wa jamii
yetu.
Kesho -Jumatatu, 2 Dec 2024* tutampuzisha
mpendwa wetu mahali penye utulivu wa milele ulioko mikononi mwa Mwenyezi Mungu
(Amen)
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
P. O. Box 6
Musoma
Tarehe:
Jumapili, 1 Dec 2024